Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 17:05

Matayarisho ya harusi ya Harry, Meghan yakamilika


Polisi wakifanya mazoezi ya maandalizi ya ulinzi ikiwa ni hatua ya kuimarisha usalama katika eneo ambalo harusi ya Harry na Meghan itafanyika
Polisi wakifanya mazoezi ya maandalizi ya ulinzi ikiwa ni hatua ya kuimarisha usalama katika eneo ambalo harusi ya Harry na Meghan itafanyika

Siku muhimu inakaribia hapa Uingereza ambapo Prince Harry na Meghan Markle, wapenzi wawili wanatarajiwa kufunga ndoa Jumamosi katika mji wa Windsor, nje ya mji wa London.

Mcheza filamu wa Marekani amethibitisha wiki hii kuwa baba yake hatoweza kushiriki sherehe hizo kutokana na kuugua, baada ya kuwepo hisia iwapo ataweza kusafiri kuvuka bahari ya Atlantic kuhudhuria harusi hiyo.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari, Thomas Markle, ambaye anaishi huko mji wa Mexico, alifanyiwa upasuaji Jumatano kutokana na maradhi ya moyo.

Watu wengi wanatarajiwa kufika katika mji huo wa kihistoria na wanaowatakia mafanikio maharusi hao wanajaribu kujua zaidi juu ya wapenzi hao katika uko wa ufalme.

Maelfu ya maafisa wa polisi wameandaliwa kuimarisha ulinzi mkubwa kuliko yote katika miaka ya hivi karibuni, ambao unalipiwa na fedha za umma, na wale wanaopinga ufalme hawakubaliana na matumizi hayo.

Wanaounga mkono wanadai kuwa kuna uwezekano kuwa harusi hiyo itawavutia wengi ambao kuja kwao kutasaidia nchi kiuchumi kwa kufanya matumizi na wale watakao kuwa wanaangalia kutoka katika vilabu vya starehe na kuwepo kwa screen kubwa ambazo zitawaleta wateja kuangalia na kufanya matumizi.

Tafrija hizo zinaanza kufanyika baada ya saa sita mchana katika Kanisa la Mtakatifu George lenye umri wa karne 14, ambapo Prince Harry alibatizwa mwaka 1984.

Takriban wageni 600 wamealikwa, hasa wale waliokuwa na mahusiano ya moja kwa moja na maharusi hao kwa kuzingatia kuwa nafasi ni ndogo katika kanisa hilo.

Kadhalika, zaidi ya raia 2500 wamealikwa kuhudhuria harusi hiyo kwenye viwanja vya kasri ya malikia – sehemu kuu ya kuangalia wale wageni wanaoingia na kutoka.

“Kwangu mimi, hilo ni jambo la kushangaza, na linafurahisha sana. Kwa sababu pamoja na kuwa hawapendi vyombo vya habari kuwepo, familia ya kifalme, wamevialika vyombo vya habari, wamewaalika wananchi na wanataka kushirikiana nao katika siku hiyo muhimu,” amesema Thomas Mace-Archer-Mills wa Jumuiya ya Wafalme wa Uingereza na Taasisi yake.

XS
SM
MD
LG