Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 02, 2022 Local time: 10:20

Mkurugenzi wa CIA apitishwa na Baraza la Seneti


Gina Haspel

Baraza la Seneti la Marekani Alhamisi limempitisha Gina Haspel kama Mkurugenzi mwanake wa kwanza wa Idara ya Ujasusi ya Marekani.

Amepitishwa kwa kura 54 dhidi ya 45, ikimaliza mchakato wa uteuzi uliokuwa na utata ambapo wabunge walidurusu njia zinazotumiwa na CIA kuwahoji washukiwa.

Wademokrati sita walipiga kura kumpitisha Haspel, wakati Warepublikan wawili walipinga uteuzi wake wa kuchukua nafasi ya Mike Pompeo aliyethibitishwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje.

Kiongozi wa waliowengi katika Baraza la Seneti Mitch McConnell, Mrepublikan wa Jimbo la Kentucky, alimpongeza Haspel, mtumishi wa muda mrefu katika CIA kuwa "anasifa za kipekee kuweza kukabiliana na changamoto za usalama wa taifa."

Pia ameongeza kuwa mwanamke huyo " amepata heshima na kukubalika kiutendaji na wanaume na wanawake wanaofanya kazi katika CIA."

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG