Balozi wa Marekani nchini Libya na wafanyakazi watatu wa ubalozi wameuliwa baada ya kundi la watu kuvamia afisi ya ubalozi mdogo wa Marekani katika mji wa mashariki wa Benghazi usiku Jumanne. J. Christopher Stevens,ni mmoja kati ya maafisa wenye ujuzi mkubwa wa mashariki ya kati katika wizara ya mambo ya kigeni.
Balozi wa Marekani Christopher Stevens

1
Chris Stevens mjumbe wa Marekani akiwa katika hoteli ya Tibesty, Bengazi ambako ujumbe wa Umoja wa Afrika ulikuwa unakutana na viongozi wa upinzani wa Libya. (April 2011 file photo)

2
John Christopher Stevens, balozi mpya wa Marekani nchini Libya, akisalimiana na mwenyekiti wa Baraza la Mpito la Kitaifa Libya (NTC) Mustafa Abdel Jalil (Kulia) baada ya kumkabidhi stakbadhi zake za uteuzi mjini Tripoli, June 7, 2012.

3
U.S. envoy Chris Stevens akizungumza na waandishi habari wa Libya katika hoteli ya Tibesty (April 2011 file photo)

4
U.S. envoy Chris Stevens, katikati, akifuatana na mjumbe wa Uingereza Christopher Prentice, kushoto, akizungumza na diwani wa Misrata Dr. Suleiman Fortia, kulia, katika hoteli ya Tibesty Benghazi.