Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 03:36

Nchi za G20 zatarajiwa kufikia makubaliano ya mageuzi ya ulipishaji kodi


Polisi wa Italia wakifanya doria katika eneo la St.Mark wakati mkutano wa G20 wa mawaziri wa fedha na magavana wa benki ukiendelea huko Venice, Italia, Alhamisi, Julai 8, 2021. (AP Photo/Luca Bruno)
Polisi wa Italia wakifanya doria katika eneo la St.Mark wakati mkutano wa G20 wa mawaziri wa fedha na magavana wa benki ukiendelea huko Venice, Italia, Alhamisi, Julai 8, 2021. (AP Photo/Luca Bruno)

Mawaziri wa fedha wa mataifa 20 tajiri duniani, G20, wanatarajiwa kufikia makubaliano yatakayoleta mageuzi katika ulipishaji kodi.

Mawaziri hao ambao wanakutana mjini Venice, Italia, Jumamosi kwa siku ya pili wanatarajiwa kuidhinisha makubaliano yatakayoleta mageuzi makubwa katika kuyalipisha makampuni ya kimataifa kodi itakayokuwa na usawa na haki zaidi.

Pendekezo la mageuzi ya ulipishaji kodi wa kimataifa utakuwa pia na kiwango cha chini cha asilimia 15 cha utozaji kodi kilichokubaliwa na mataifa 131 mapema mwezi Julai.

Lengo la mageuzi hayo ni kuzuia uwezekano wa kuwepo viwango vya chini zaidi vya kutoza kodi wakati mataifa yanajaribu kuvutia uwekezaji wa makampuni mkubwa. Makampuni hayo ya kimataifa yanawekeza katika nchi zenye kodi ya chini zaidi ili kukwepa kulipa kodi za juu katika nchi zao.

Waziri wa Fedha wa Ufaransa Bruno Le Maire aliliambia shirika la habari la AFP kwamba mawaziri wakikubaliana juu ya mkataba huo basi ulipaji kodi huo wa kiwango cha chini kufuatana na mkataba utaanza kutekelezwa mwaka 2023.

Marekani na Ujeriumani na baadhi ya nchi zinataka kuwepo na kiwango cha juu zaidi.

Chanzo cha Habari : AFP

XS
SM
MD
LG