Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 07:56

WB, na IMF zasihi mataifa tajiri kusamehe madeni ya nchi masikini


Benki ya dunia yenye makao yake makuu Washington DC, Marekani
Benki ya dunia yenye makao yake makuu Washington DC, Marekani

Rais wa benki ya dunia, David Malpass, Jumatatu amesema baadhi ya wakopeshaji kutoka nchi zilizoendelea kiuchumi maarufu kama G20, bado wanasita kurefusha kwa mwaka mmoja, kipindi cha kusamehe madeni kwa nchi maskini zilizoathiriwa na janga la virusi vya corona.

Kiongozi huyo wa benki ya dunia amesema huenda wiki hii wakopeshaji hao wakaafikiana kuzisamehe nchi maskini kulipa madeni kwa kipindi cha miezi sita.

Akizungumza na waandishi wa habari, Malpass, amesema wakopeshaji wa G20 hawajafikia makubaliano kuhusu pendekezo la benki ya dunia na shirika la kimataifa la fedha IMF, la kurefusha kipindi cha mwaka mmoja kwa mataifa masikini yaweze kulipa madeni yao.

Mawaziri wa fedha na wakuu wa benki za taifa kutoka kundi la G20, wanatarajiwa kukutana kesho jumatano kwa njia ya mtandao, ili kuchukua maamuzi.

Wakati huohuo shirika la kimataifa la fedha-IMF, Jumatatu limesema kwamba jumuia ya kimataifa inatakiwa kuongeza juhudi katika kukabiliana na athari za kiuchumi za janga la Covid-19.

IMF pia imetoa rasmi wito kwa benki ya dunia kuendelea kutoa mkopo kwa mataifa ya Afrika yalioathiriwa na janga la corona.

Tutaendelea kuhamasisha ili hatua zaidi zichukuliwe,” mkurugenzi wa IMF, Kristalina Georgieva, amesema katika mkutano wa biashara wa mataifa ya Afrika kwa njia ya mtandao.

Ameongeza kuwa ataendelea kuomba misaada zaidi ya pesa itolewe kwa nchi za Afrika.

Wiki iliopita, Georgieva, alisema kwamba IMF ilitoa mkopo wa dola billioni 26 kwa serekali za Afrika tangu litokee janga la virusi vya corona, lakini kutokana na uhaba wa mikopo ya sekta binafsi, bara la Afrika litakua na pengo la ufadhili wa dola billioni 345 ifikapo mwaka wa 2023.

XS
SM
MD
LG