Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 21, 2023 Local time: 07:06

Saudi Arabia mwenyeji wa mkutano wa kwanza wa mtandao wa G-20


Mfalme wa Saudi Arabia, Salman bin Abdulaziz akitoa hotuba kwa njia ya video wakati wa ufunguzi wa G20

Mkutano huo unafanyika kwa mara ya kwanza kwa njia ya mtandao mwaka huu kwa sababu ya janga la COVID-19. Washiriki wanatarajiwa kujadili athari za ugonjwa wa virusi vya Corona kwenye uchumi wa Dunia na kutathmini njia za kuchochea kufufua pamoja na ukuaji wa uchumi

Saudi Arabia ni mwenyeji wa mkutano unaofanyika kwa njia ya video, Jumamosi na Jumapili wa kundi la G-20 la mataifa yaliyoendelea na yale yanayoinukia kiuchumi duniani. Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kushiriki katika mkutano huo kwa siku zote mbili, kulingana na White House.

Mkutano huo unafanyika kwa mara ya kwanza kwa njia ya mtandao mwaka huu kwa sababu ya janga la COVID-19. Washiriki wanatarajiwa kujadili athari za ugonjwa wa virusi vya Corona kwenye uchumi wa Dunia na kutathmini njia za kuchochea kufufua pamoja na ukuaji wa uchumi.

Saudi G20
Saudi G20

Wafuatiliaji wanasema hata hivyo inawezekana kwamba wakati wa mkutano huo wa uchumi baadhi ya viongozi wa ulimwengu watakabiliana na mwenyeji wa mkutano huo Mwana mfalme Mohammed bin Salman juu ya mauaji ya mwandishi wa Habari Jamal Khashoggi ambaye aliripotiwa kuuawa nchini uturuki na wakala wa Saudi Arabia.

Nchi wanachama wa G-20 ni pamoja na Afrika kusini, Argentina, Australia, Brazil, Uingereza, Canada, China, Ufaransa, Ujerumani, India. Nyingine ni Indonesia, Italy, Japan, Mexico, Russia, Saudi Arabia, Korea kusini, Uturuki, Marekani na Umoja wa Ulaya.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG