Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 18:05

Wakazi wa Puerto Rico waanza kurejea majumbani


Madhari ya kimbunga Maria huko Puerto Rico.
Madhari ya kimbunga Maria huko Puerto Rico.

Gavana wa Puerto Rico, Ricardo Rossello amesema Jumapili kwamba idadi ya wa-Puerto Rico walioko kwenye makazi ya muda imepungua sana baada ya janga la kimbunga Maria.

“Jumla ya watu katika makazi ya muda imepungua. Tuna kiasi cha wakimbizi 8,800 wakati huu na makazi ya muda 139 alisema hayo akielezea kwamba wiki moja iliyopita kulikuwa na nyumba za muda 500 kote kisiwani humo. Tunajiimarisha kuhakikisha watu wanarudi kwenye nyumba zao na wale wasioweza kurudi kwenye nyumba zao tunawapatia nyumba mbadala kwa wakati huu,” amesema Gavana.

Gavana wa Puerto Rico, Ricardo Rossello
Gavana wa Puerto Rico, Ricardo Rossello

Rossello pia alisema kwamba wanajeshi kadhaa wa wizara ya ulinzi Marekani waliopo huko waliongezeka kufikia 6,400 Jumapili kutoka 4,600 saa 36 za mwanzo. Takribani wiki moja na nusu baada ya kimbunga Maria kupiga Puerto Rico kiasi cha nusu ya wakazi milioni 3.4 kwenye kisiwa hicho bado wana ukosefu wa fursa ya maji safi ya kunywa kwa mujibu wa wizara ya ulinzi Marekani wakati asilimia 95 hawana umeme.

Gavana Rossello alieleza kwamba nafuu imepatikana. Alisema hospitali 51 kati ya 60 kwenye kisiwa hicho zipo wazi na viwanja vya ndege na bandari zinapokea mizigo.

XS
SM
MD
LG