Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 26, 2024 Local time: 11:02

Mtoto wa Gadhafi kuwania urais wa Libya


Mwana wa Moammar Gadhafi,Saif al-Islam al-Gaddafi,wakati akijiandikisha kugombea urais Jumapili
Mwana wa Moammar Gadhafi,Saif al-Islam al-Gaddafi,wakati akijiandikisha kugombea urais Jumapili

Mtoto  wa kiume wa marehemu kiongozi wa Libya Moammar Gadhafi Jumapili amejitokeza hadharani kwa mara ya kwanza baada ya zaidi ya muongo mmoja.

Gadhafi alionekana wakati akijiandikisha kama mgombea wa urais kwenye uchaguzi mkuu wa Decemba unaolenga kumaliza miaka mingi ya ghasia tangu baba yake alipoondolewa madarakani.

Saif al Islam al Gadhafi mwenye umri wa miaka 49 alionekana kwenye video ya tume ya kitaifa ya uchaguzi huku akiwa amevaa gwanda la kitamaduni pamoja na kitambaa cha kichwa akionekana mwenye ndevu nyeupe pamoja na miwani, wakati akitia saini kwenye nyaraka katika mji mkuu wa kusini wa Sebha.

Gadhafi ni mmoja wa watu mashuhuri na mwenye utata kwenye orodha ya uchaguzi huo ambayo pia inajumuisha kamanda wa jeshi Khalifa Haftar, waziri mkuu Abdulhamid al Dbeibah pamoja na spika wa bunge Aguila Saleh.

Mkutano wa Ijumaa mjini Paris ulikubaliana kumuadhibu yeyote atakayejaribu kuhujumu uchaguzi wa Libya, lakini wakati zikiwa imebaki chini ya wiki sita kabla ya zoezi hilo kukamilika, bado hakuna makubaliano ya sheria na ratiba zitakazo tumika.


XS
SM
MD
LG