Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 19, 2024 Local time: 00:29

Libya yajitayarisha kwa uchaguzi mkuu


Wapiganaji wa kundi la Misrata wakitayarisha silaha zao [Maktaba]
Wapiganaji wa kundi la Misrata wakitayarisha silaha zao [Maktaba]

Serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya, inayokumbwa na misukosuko, imeandaa kongamano la kimataifa hii leo kwa lengo la kutafuta uungwaji mkono wakati nchi hiyo inayokumbwa na vita inapojitayarisha kwa uchaguzi mkuu mwezi Desemba mwaka huu.

Kongamano hilo linalofanyika kwa kuzingatia mpango wa amani unaoongozwa na umoja wa mataifa, linafanyika miezi miwili kabla ya uchaguzi huo mkuu wa urais.

Akifungua mkutano huo, kiongozi wa serikali ya mpito Abdelhamid Dbeibah, amesema kuwepo kwa maafisa wa ngazi za juu wa kimataifa ni dhihirisho tosha kwamba uchaguzi mkuu utafanyika namna ulivyopangwa na kutaka wagombea kukubali matokeo.

Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anaeshughulikia masuala ya kisiasa Rosemary DiCarlo, amesisitiza umuhimu wa uchaguzi huo wa mwezi Desemba akisema utakamilisha mchakato wa kuundwa kwa serikali nchini humo.

Ametoa wito kwa mashirika ya kimataifa kutuma wajumbe maalum kufuatilia uchaguzi huo ili kuhakikisha kwamba unafanyika katika mazingira yaliyo huru na haki.

Nchi zenye nguvu duniani zimekuwa zikishnikiza Libya kuandaa uchaguzi mkuu katika mda uliopangwa baada ya tarahe ya uchaguzi kukubaliwa katika mazungumzo yaliyoongozwa na umoja wa mataifa mwaka uliopita.

Lakini mchakato wa kuandaa uchaguzi huo umekumbwa na hali ya kutoelewana hasa kuhusiana na iwapo unaandaliwa kulingana na sheria.

Uchaguzi wa urais umepangiwa kufanyika Desemba 24. Uchaguzi wa bunge umecheleweshwa na tarahe itaamuliwa mwaka ujao.

Viongozi wa Libya na umoja wa mataifa, wamekuwa wakijaribu kugeuza ukurasa mpya katika historia ya nchi hiyo kwa kukomesha vita ambavyo vimeikumba tangu mwaka 2011, pale wanajeshi wa NATO walipoongoza mapinduzi ya serikali na kuuawa kwa Moamer Gadhafi.

Hatua ya kusitisha mapigano kati ya makundi ya wapiganaji ya mashariki na magharibi mwa nchi hiyo, ilipelekea kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa mwezi March.

Serikali hiyo ya umoja wa kitaifa ina jukumu la kuandaa uchaguzi mkuu.

XS
SM
MD
LG