Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:33

Mlipuko wa kipindupindu waikumba DRC


Wagonjwa wakitibiwa kutokana na kipindupindu katika hospitali ya Mkoa wa Bukavu, Kivu Kusini Agosti 16, 2017. (VOA/Ernest Muhero)
Wagonjwa wakitibiwa kutokana na kipindupindu katika hospitali ya Mkoa wa Bukavu, Kivu Kusini Agosti 16, 2017. (VOA/Ernest Muhero)

Watu tisa wamefariki katika jimbo la Haut-Lomami, jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kutokana na mlipuko wa kipindupindu.

Madaktari wasiokuwa na mipaka wameonya kwamba huenda watu wengi zaidi wakafariki kwa kukosa huduma za msingi za afya hasa katika eneo la Mulongo.

Madaktari wasiokuwa na mipaka wameweka kituo vya matibabu chenye vitanda 30, katika eneo la Kabamba ambako ndio kitovu cha maambukizi ya kipindipindu.

Vituo vingine viwili vya kutibu kipindupindu vimewekwa Ngoya na Bukena ili kudhibiti maambukizi.

Eneo hilo la Mulongo linakabiliwa na uhaba mkubwa wa maafisa wa afya pamoja na vifaa vya matibabu.

Maafisa wa afya wamesema kwamba mlipuko wa kipindupindu wa sasa haujawahai kutokea katika sehemu hiyo ya Mulongo tangu kutokea milipuko mikubwa ya m waka 2017 na 2019.

Mratibu wa shughuli za madaktari wasio na mipaka katika jimbo la Haut Lomami, Clement Shap, ameomba msaada kutoka kwa mashirika mengine, akisema kwamba mahitaji ya sasa kukabiliana na ugonjwa huo kusambaa, hayawezi kutoshelezwa na madaktari hao pekee.

Clement amesema kwamba vituo vya afya vya Mulongo vimezidiwa na wagonjwa na haviwezi kudhibithi maambukizi hayo ya kipindupindu.

XS
SM
MD
LG