Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 08, 2023 Local time: 02:55

Wafanyakazi watatu wa UNHCR wajeruhiwa kwa shambulizi huko DRC


Mfano wa kazi zinazofanywa na UNHCR
Mfano wa kazi zinazofanywa na UNHCR

Timu hiyo ya wafanyakazi ilikuwa ikirejea katika mji wa Beni baada ya kusambaza misaada kwa watu ambao tayari wamekimbia makaazi yao kutokana na ghasia na walikuwa wakitumia gari lililosomeka vyema maandishi yake UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) lilisema Alhamis kwamba Wafanyakazi wake watatu walijeruhiwa katika shambulizi lililotokea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Washambuliaji wasiojulikana walifyatua risasi kwenye msafara wa Umoja wa Mataifa uliokuwa ukisafiri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, UNHCR ilisema katika taarifa yake. Risasi zilipiga gari na wafanyakazi watatu walijeruhiwa, kwenye shambulizi la Jumatano. Shambulizi hilo lilitokea katika eneo la Mambassa, eneo la Lubero, jimbo la Kivu kaskazini, ilisema taarifa hiyo.

Mfano wa magari yenye nembo za UNHCR
Mfano wa magari yenye nembo za UNHCR

Wafanyakazi waliojeruhiwa walikuwa wakisafiri kwa gari lililokuwa na alama zinazoonekana vyema za UNHCR. Timu hiyo ilikuwa ikirejea katika mji wa Beni, baada ya kusambaza misaada kwa watu ambao tayari wamekimbia makaazi yao kutokana na ghasia na kwa familia zilizo hatarini kutoka kwa jamii inayowapokea.

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa limesema limeshtushwa na kukasirishwa na shambulizi hilo, na linatoa wito kwa maneno makali zaidi kuheshimiwa kwa sharia ya kimataifa ya kibinadamu na haki za binadamu ili kuwalinda raia na wafanyakazi wanaotoa msaada wa kibinadamu dhidi ya ghasia.

XS
SM
MD
LG