Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 08, 2023 Local time: 07:24

Mfumuko wa bei Ghana wapandisha gharama za huduma mbalimbali


Rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo (AP)

Kiwango cha mfumuko wa bei nchini Ghana kimeongezeka mpaka asilimia 50.3 mwezi Novemba, kikiwa kimepanda kutoka asilimia 40.4  mwezi mmoja kabla, kwa mujibu wa takwimu za karibuni zilizotolewa na idara ya takwimu Ghana.

Hiki ni kiwango kikubwa sana kurekodiwa katika kipindi cha zaidi ya miongo miwili.

Hii inahusishwa na kupanda sana kwa gharama za nyumba, umeme, maji, gesi na mafuta ya aina nyingine, ambazo zilirekodo kiwango cha juu cya mfumuko wa bei mpaka asilimia 79.

Jumanne, Ghana ilifikia mkataba wa awali huko IMF kwa kupatiwa dola bilioni 3 za kuwasaidia kupata idhini ya bodi ya shirika hilo la kimataifa la fedha kama nchi itakidhi mahitaji yote yaliyowekwa.

Makubaliano yalitarajiwa kusaidia kurejesha uthabiti wa kiuchumi wa Ghana na kuhakikisha uendelevu wa deni.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG