Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 23:36

Ghana yajiweka katika nafasi nzuri baada ya ushindi  dhidi ya Korea Kusini


Daniel Amartey, kulia, akishangilia na wachezaji wenzake mwishoni mwa mechi ya kandanda ya Kundi H ya Kombe la Dunia kati ya Korea Kusini na Ghana, kwenye Uwanja wa Education City mjini Al Rayyan, Qatar, Jumatatu, Novemba 28, 2022. AP.
Daniel Amartey, kulia, akishangilia na wachezaji wenzake mwishoni mwa mechi ya kandanda ya Kundi H ya Kombe la Dunia kati ya Korea Kusini na Ghana, kwenye Uwanja wa Education City mjini Al Rayyan, Qatar, Jumatatu, Novemba 28, 2022. AP.

Timu ya Ghana imefanikiwa kupata ushindi muhimu katika kombe la dunia baada ya kuifunga Korea Kusini bao 3-2.

Wawakilishi hao wa Afrika Ghana wamefanikiwa kupata ushindi wao wa kwanza katika kombe la Dunia mwaka huu

Ghana ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Salisu Mohamed katika dakika ya 24 na kuongeza bao la pili dakika 10 baadaye kupitia kwa Mohamed Kudus na mpaka mapumziko Ghana ilikuwa inaongoza bao 2-0.

Katika kipindi cha pili Korea Kusini walishambulia kama nyuki na kufamnikiwa kurusidisha mabao yote mawili ndani ya dakika 3 kupitia kwa mshambuliaji Gue -Sung Jo kunako dakika ya 58 na 61.

Na mpira ukawa droo , lakini Ghana waliongeza mashambulizi na hatimaye kufanikiwa kupata bao la tatu na la ushindi katika dakika ya 68 kuitia Mohamed Kudus tena.

Katika dakika za mwisho Korea kusini ilishambulia kwa nguvu sana ngome ya Ghana ambayo ilionekana kutikiswa na mashambulizi hayo lakini walifanikiwa kumaliza mchezo huo kwa ushindi uliohitajika sana kwao.

Cameroon yatoka sare na Serbia

Timu ya Cameroon ilitoka sare ya bao 3-3 na timu ya Serbia katika mchezo mkali wa kundi G katika uwanja wa Al janoub siku ya Jumatatu

Mchezo huo ulioshuhudiwa kuwa wa kuvutia na ushindani mkubwa Cameroon wakionyesha mabadiliko makubwa hasa baada ya kuingizwa kwa mshambuliaji Vincent Abubakar wakiwa nyuma kwa magoli matatu kwa moja.

Abubabakar alipachika bao la pili na kutoa asisti ya bao la 3. Itakumbulwa kuwa Abubakar alichukua kiatu cha dhahabu akiwa mfungaji bora wa timu ya Cameroon katika michuano ya kombe la mataifa ya Afrika 2021.

Moja ya magoli bora ya World cup ambayo yameshuhudiwa ni goli la pili la Cameroon lake Vincent Abubakar alipompiga chenga kali beki wa Serbia na kuingiza mpira nyavuni kwa kuudokoa juu ya golikipa wa Serbia na kutinga nyavuni.

Ureno yasonga mbele

Na timu ya Ureno imefanikiwa kusonga mbele katika raundi ya 16 baada ya kuifunga Uruguay bao 2-0 katika uwanja wa Lusaille mjini Doha Qatar.

Alikuwa ni mshambuliaji wa Ureno na Manchester United Bruno Fernandes aliyefunga mabao hayo mawili katika dakika ya 54 na katika dakika za majeruhi kwa njia ya penati.

Uruguay kwa upande wao walikosa nafasi kadhaa za wazi katika mchezo huo kupitia wachezaji Edson Cavani na Luis Suarez.

Uruguay sasa ina pointi moja tu katika mechi mbili na inahitaji kuishinda Ghana Ijumaa ili kujiweka katika nafasi ya kusonga mbele.

Brazil yasonga mbele

Nayo timu ya Brazil imesonga mbele katoka raundi ya pili baada ya kuifunga Uswissi bao 1-0 katika uwanja wa 974 mjini Doha Qatar.

Alikuwa ni mchezaji mkongwe wa timu hiyo Carlos Henrique aliyepachika bao la pekee na la ushindi kunako dakika ya 83 na kuikatia Brazil tiketi ya kwenda raundi ya pili.

Mabingwa watetezi Ufaransa wamekuwa timu ya kwanza kutinga hatua ya 16 bora baada ya kupata ushindi dhidi ya Denmark siku ya Jumamosi, huku Brazil na Ureno wakiungana nao, hivyo kuacha nafasi 14 kunyakua katika vita vya kuwania taji hilo maarufu la kandanda.

Qatar sio timu pekee iliyoondoka kwenye michuano hiyo baada ya michezo miwili pekee, huku Canada iliyokuwa na mashabiki wengi pia kushindwa baada ya kusambaratishwa na washindi wa pili wa fainali za 2018, Croatia siku ya Jumapili na kuwaacha wakiwa mkiani mwa Kundi F.

XS
SM
MD
LG