Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 14:07

Mfalme wa Ubelgiji arejesha turathi ya asili ya utamaduni wa Congo


Mfalme wa Ubelgiji Philippe (Kushoto) akiwa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi (Kulia) alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa e N'djili Kinshasa, June 7, 2022. (Photo by Arsene Mpiana / AFP)
Mfalme wa Ubelgiji Philippe (Kushoto) akiwa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi (Kulia) alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa e N'djili Kinshasa, June 7, 2022. (Photo by Arsene Mpiana / AFP)

Mfalme wa Ubelgiji Phillipe amerejesha turathi ya asili ya kitamaduni huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Jumatano katika ziara yake ya kwanza kwenye koloni lake la zamani.

Katika nchi hiyo watu wengi bado wana hasira kuhusu Ubelgiji kushindwa kuomba radhi kwa miongo kadhaa ya utawala wake wa kikatili.

Kwa makadirio kadhaa, mauaji, ukame, na magonjwa yameuwa watu karibu milioni kumi wa Congo wakati wa miaka 23 ya kwanza ya utawala wa Ubelgiji kuanzia mwaka 1885 hadi 1960 baada ya Mfalme Leopold wa pili kudai Congo kuwa milki yake binafsi.

Mwaka 2020 Philippe alikuwa afisa wa kwanza wa Ubelgiji kujutia mateso na fedheha iliyosababishwa kwa Congo.

Lakini hakuomba msamaha na baadhi ya Wakongo wamemtaka afanye hivyo katika ziara hii ya kwanza tangu achukue kiti cha Ufalme mwaka 2013.

Rais wa Congo Felix Chisekedi na wanasiasa wengi wamekaribisha ziara yake kwa furaha na wakaazi wengine wana matumaini kwamba inaweza kuleta uwekezaji na mwelekeo mpya wa kulenga ghasia mashariki mwa nchi.

Mfalme aliwasili Jumanne na mkewe, Malkia Mathilde na Waziri Mkuu Alexander De Croo katika ziara ya wiki moja ambayo pia itampeleka katika miji ya mashariki ya Bukavu na Lubumbashi.

XS
SM
MD
LG