Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 04:04

Maandamano DRC kutokana na madai ya Rwanda kuunga mkono waasi wa M23


Wanajeshi wa DRC wakishirkiana na walinda usalama wa umoja wa mataifa (MONUSCO) katika msako dhidi ya waasi wa M23 PICHA: Austere Malivika.
Wanajeshi wa DRC wakishirkiana na walinda usalama wa umoja wa mataifa (MONUSCO) katika msako dhidi ya waasi wa M23 PICHA: Austere Malivika.

Mamia ya watu wamejitokeza kwenye maandamano mjini Kinshasa, Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, kuonyesha hasira yao kutokana na shutuma kuwa Rwanda inawaunga mkono waasi wa M23.

Maandamano yameandaliwa na kundi la kuetetea haki za kiraia la NDSCI.

Jumatatu, mwenyekiti wa umoja wa Afrika, ambaye ni rais wa Senegal Macky Sall, aliwasiliana kwa njia ya simu na rais Paul Kagame wa Rwanda na Felix Tshisekedi wa DRC, katika hatua za kupunguza mgogoro kati ya nchi hizo mbili.

DRC na Rwnada zinashutumiana kwa kuunga mkono makundi ya waasi mashariki mwa DRC.

Sall, alielezea wasiwasi kutokana na mgogoro unaoongezeka kati ya Rwanda na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Amewataka viongozi wa nchi hizo mbili kujadiliana na kutatua mgogoro huo.

Rais wa Angola João Lourenço, amesema kwamba Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imekubali kuwaachilia wanajeshi wawili wa Rwanda waliokamatwa na wanajeshi wa DRC wiki iliyopita, huku hali ya wasiwasi ikiendelea kuongezeka mpakani.

Lourenço – ambaye anakaimu kama mpatanishi kati ya Rwanda na DRC, amesema kwamba Tshisekedi na Kagame wamekubaliana kukutana kwa mazungumzo ya ana kwa ana, bila ya kutoa tarehe kamili ya mkutano huo.

DRC inadai kwamba Rwanda inaunga mkono waasi wa M23, huku Rwanda ikidai kwamba DRC inaunga mkono waasi wa FDLR.

XS
SM
MD
LG