Ni ghasia za hivi karibuni katika mzozo huo wa muda mrefu ambao uliibuwa katika wiki za hivi karibuni na kusababisha mvutano wa kidiplomasia na nchi jirani ya Rwanda.
Waasi wa M23 walishambulia kwa makombora kituo cha jeshi huko Kivu Kaskazini, na kuua wanajeshi wawili na kujeruhi wengine watano.
Congo inamshtumu jirani yake kuunga mkono kundi la M23, tuhuma ambazo Rwanda inakanusha.
Mapigano hayo yanafuatia uvamizi uliofanywa Jumapili kwenye kijiji cha mkoa jirani wa Ituri na wapiganaji wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa kiislamu kutoka kundi lingine la uasi na kuua watu 18, vyanzo vya eneo hilo vimesema.
Wapiganaji wanaoshukiwa kuwa wa kundi la Alliance Democratic Forces (ADF) waliua wakazi na kuchoma moto nyumba katika kijiji cha Otamabere, wamesema, shahidi mmoja, kiongozi mmoja na shirika la haki za binadamu katika eneo hilo.
Msemaji wa jeshi la Congo Jules Ngongo amethibitisha shambulizi la ADF bila kutoa idadi ya vifo.