Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 17:04

Uganda na DRC zimeongeza muda wa shughuli za Operesheni Shujaa


DRC na Uganda zimetia saini kuongeza muda wa ufanyaji kazi za pamoja katika Operesheni Shujaa
DRC na Uganda zimetia saini kuongeza muda wa ufanyaji kazi za pamoja katika Operesheni Shujaa

Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) Jumatano ziliongeza operesheni ya pamoja ya kijeshi iliyoanzishwa mwishoni mwa mwaka jana dhidi ya waasi wa kiislam mashariki mwa Congo msemaji wa operesheni hiyo alisema.

Nchi ya Uganda ilituma takribani wanajeshi 1,700 kwa jirani yake wa Afrika ya kati hapo mwezi Disemba ili kusaidia kupambana na kundi la waasi lenye vurugu linalojulikana kama Allied Democratic Forces (ADF) uingiliaji mkubwa zaidi wa kigeni nchini Congo katika kipindi cha muongo mmoja kando na operesheni ya kulinda Amani ya Umoja wa mataifa.

Hapo awali ilikusudia kudumu kwa miezi sita. Operesheni Shujaa iliongezwa siku ya Jumatano licha ya tangazo la awali lililotolewa na jeshi la Uganda kwamba lingeondoa wanajeshi mara operesheni hiyo itakapokamilika kinyume na hapo kama itaelekezwa vinginevyo.

Msemaji wa Shujaa, Kanali Mak Hazukay aliliambia shirika la habari la reuters kuwa majeshi ya Congo na Uganda yalitia saini Juni mosi kuongeza muda wa operesheni zao za kijeshi katika awamu ya tatu, kwa sababu tishio hilo halijatokomezwa.

XS
SM
MD
LG