Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 29, 2023 Local time: 17:22

Meli ya starehe iliyokwama Lisbon kutokana na Covid yaondoka


Picha ya meli ya safari za kifahari. (AP Photo/John Raoux)
Picha ya meli ya safari za kifahari. (AP Photo/John Raoux)

Meli ya safari za starehe inayoendeshwa na kampuni ya Ujerumani, ambayo ilikuwa imekwama katika bandari ya Lisbon baada ya kuzuka mlipuko wa virusi vya corona kwa mabaharia hatimaye imeondoka.

Hatua hiyo ni baada ya baadhi ya abiria kugundulika wameambukizwa Covid kwa mujibu wa mamlaka ya bandari.

Meli ya AIDAnova, ikiwa na abiria 2,844, na mabaharia 1,353 ilitia nanga Lisbon, Disemba 29 ikiwa njiani kuelekea kisiwa cha Madeira kwa ajili ya kusherehekea mkesha wa mwaka mpya, ilishindwa kuendelea na safari baada ya kugundulika maambukizo 52 ya Corona kwa watu waliokuwa wamechanjwa kikamilifu Covid-19.

Imeruhusiwa kuondoka bandarini hapo na kuelekea katika kisiwa cha Uhispania cha Lanzarote Jumapili, lakini watu 12 zaidi wamegundulika kuwa na maambukizi ikijumuisha abiria wanne alisema nahodha wa meli hiyo. Abiria watasafirishwa kurejea makwao kwa ndege aliongeza kusema licha ya kutotoa taarifa zaidi.

XS
SM
MD
LG