Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:49

Ulaya yavuka kesi milioni 100 za virusi vya corona tangu janga lililpoanza


Watu wakishehekea wakati wa Mkesha wa Mwaka Mpya, huko Belgrade, Serbia. Sherehe za Mkesha wa Mwaka mpya zilifanyika Serbia Belgrade tofauti na kwingineko barani Ulaya, ambako mikusanyiko ya watu wengi iliruhusiwa licha ya ongezeko la maambukizi ya corona, aina ya Omicron.
Watu wakishehekea wakati wa Mkesha wa Mwaka Mpya, huko Belgrade, Serbia. Sherehe za Mkesha wa Mwaka mpya zilifanyika Serbia Belgrade tofauti na kwingineko barani Ulaya, ambako mikusanyiko ya watu wengi iliruhusiwa licha ya ongezeko la maambukizi ya corona, aina ya Omicron.

Ulaya imevuka kesi milioni 100 za virusi vya corona tangu janga lililpoanza karibu miaka miwili iliyopita, kwa mujibu wa takwimu kutoka kituo cha John Hopkins cha virusi vya corona. Kote duniani, takriban kesi milioni 290 zimerekodiwa

Ulaya imevuka kesi milioni 100 za virusi vya corona tangu janga lililpoanza karibu miaka miwili iliyopita, kwa mujibu wa takwimu kutoka kituo cha John Hopkins cha virusi vya corona. Kote duniani, takriban kesi milioni 290 zimerekodiwa.

Takriban kesi milioni 5 huko Ulaya zimeripotiwa katika muda wa siku saba zilizopita, katika. Nchi 17 kati ya 52 au maeneo ambayo yanajumuisha bara la Ulaya na kuweka rekodi ya kesi mpya kwa siku moja, kutokana na virusi vya omicron ambavyo vinaambukiza kwa kasi, shirika la habari la AFP limeripoti Jumamosi.

Zaidi ya keshi milioni 1 kati ya hizo ni zile zilizoripotiwa nchini Ufaransa, ambayo imejiunga na Marekani, India, Brazil, Uingereza na Russia na kuwa nchi ya sita kuthibitisha zaidi ya kesi kesi milioni tangu janga la virusi lilipoanza, shirika la habari la Reuters limeripoti.

Wizara ya Afya ya India imeripoti kesi mpya 22,775 za virusi vya corona siku ya Jumamosi, ikisema kesi mpya zinafikisha hesabu ya virusi nchini humo mpaka 1,431. Maafisa wa afya ya umma, hata hivyo, wameonya kwamba idadi ya kesi za Covid huenda hesabu zako ziko chini.

Gazeti la Sydney Morning Herald limeripoti Jumamosi kwamba maafisa wa afya katika jimbo la New South Wales nchini Australia ‘limevunja rekodi’ ya viwango kwa. Usiku mmoja, na kuwa moja ya usiku uliokuwa na shughuli nyingi sana katika muda wa miaka 126, wakati virusi vya omicron vikienea kote ulimwenguni.

Wakati huo huo kituo cha televisheni cha CNN kinaripoti kwamba zaidi vyuo vikuu na vyuo vingine 30 vimebadili tarehe ya masomo yao ya majira ya spring kutokana na virusi vya omicron kusambaa kote nchini Marekani.

Kituo kinachofuatilia virusi vya corona cha Johns Hopkins kimeripoti Jumamosi zaidi ya kesi milioni 289 za Covid 19 kote ulimwenguni tangu janga lilipoanza. Kituo kimesema chanjo bilioni 1.9 zimetolewa.

Baadhi ya habari katika ripoti hii zimetolewa kwa hisani ya mashirika ya habari ya Reuters na AFP.

XS
SM
MD
LG