Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 19:57

Afrika Kusini yaondoa amri ya kutotoka nje usiku


FILE — Sandile Cele, mtafiti kwenye Taasisi ya Afya ya Afrika mjini Durban, South Africa, akichunguza aina ya virusi vipya vya omicron vinavyotokana na COVID-19 Dec. 15, 2021.(AP Photo/Jerome Delay, File)
FILE — Sandile Cele, mtafiti kwenye Taasisi ya Afya ya Afrika mjini Durban, South Africa, akichunguza aina ya virusi vipya vya omicron vinavyotokana na COVID-19 Dec. 15, 2021.(AP Photo/Jerome Delay, File)

Afrika Kusini imeondoa amri ya kutotoka nje usiku maafisa wamesema kwamba nchi imevuka kipindi chenye maambukizo zaidi ya COVID-19.

Taarifa ya serikali imesema maambukizo ya Omicron ambayo yanasambaa kwa haraka yameonyesha kiwango kidogo cha watu kulazwa hospitali kuliko mawimbi ya awali.

Hata hivyo kumekuwepo na ongezeko kidogo la idadi ya vifo. Kirusi cha Omicron kwa mara ya kwanza kiliripotiwa Afrika Kusini mwezi uliopita kinasambaa kwa kasi katika maeneo mengine.

WHO ilionya kuwa mawimbi ya maambukizo ya virusi vya Delta na Omicron yanaweza kuathiri mifumo ya afya.

Lakini nchini Afrika Kusini taarifa iliyotolewa baada ya kikao maalum cha baraza la mawaziri imesema kesi na kiwango cha watu kulazwa hospitali kimeshuka karibu katika majimbo yote ya nchi .

Waziri katika ofisi ya Rais Mondli Gungubele, anaeleza: “Kwa mujibu wa wataalamu, omicron imefikia kiwango cha juu na baada ya kufikia kilele na katika masuala ya kliniki haisababishi tahadhari yoyote kwa hali kwenye hospitali.

Kulingana na wataalamu, hali inaturuhusu tuondowe masharti ya amri ya kutotoka nje. Na tayari nimeshaeleza baadhi ya mambo muhimu nchini yanayosabisha hali ambayo inataka kila mtu achukue fursa inayotuwezesha kufungua uchumi.”

katika wiki iliyomalizika ya desemba 25 mwaka huu, idadi ya maambukizo yaliyothibitishwa ilikuwa zaidi ya 89,000 chini ya zaidi ya 120,000 wiki kabla ya hapo.

XS
SM
MD
LG