Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 10:52

Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Marekani Tlaib atoa sababu za kutozuru Israeli


Mbunge Ilhan Omar, Kulia, na Mbunge Rashida Tlaib
Mbunge Ilhan Omar, Kulia, na Mbunge Rashida Tlaib

Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Marekani, Rashida Tlaib amebadilisha uamuzi wake wa kuzuru Ukingo wa Magharibi, masaa machache baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani kusema itamruhusu kuzuru Palestina kumuona bibi yake “kwa sababu za ubinadamu.”

Katika ujumbe wa Tweet Ijumaa asubuhi Tlaib alisema, “Itaniumiza sana.”

“Uamuzi huu unatokana na kuzingatia kuwa kumtembelea bibi yangu chini ya hali hizi kandamizi ni kinyume cha kile ambacho nina imani nacho – vita dhidi ubaguzi, ukandamizaji na dhulma.” Tlaib aliandika katika barua aliyoituma kwa waziri wa mambo ya ndani wa Israeli (Aryeh Deri) Alhamisi, Akiomba kuruhusiwa kumuona bibi yake, akisema ingekuwa fursa ya mwisho kumuona. Katika barua yake, Tlaib amesema ataheshimu “makatazo yote na hatahamasisha migomo dhidi ya Israel.”

Mapema Ijumaa Israel ilibadilisha msimamo wake kuhusu wabunge wanawake wawili wa Marekani ambao iliwazuilia kuingia nchini humo.na kuruhusu mmoja wa wabunge hao ,Tlaib, kuingia nchini humo.

Barua iliyoandikwa na ofisi ya wizara ya mambo ya ndani ya Israel, inasema mbunge Tlaib, atalazimika kuheshimu vizuizi vyovyote atakavyowekewa na hataruhusiwa kueneza misimamo pingamizi wakati wa ziara yake.

Hivi karibuni Rais wa Marekani Donald Trump alikuwa amekanusha madai ya kuishawishi Israel kuwazuia Tlaib na Ilhan Omar kuingia Israel.

Tlaib na Omar ni wakosoaji wakubwa wa namna Israel inavyoichukulia Palestina.

Rais Trump, alisema Alhamisi kwamba haihimizi wala kuikataza Israel kuwazuia waakilishi hao wa chama cha Democratic Ilhan Omar na Rashida Tlaib kuingia katika mipaka yake.

Trump hakutaja mtu aliyezungumza naye katika serikali ya Israel.

Akitumia ukurasa wake wa twitter, Trump alionekana kutoa changamoto kwa Israel, kabla ya maamuzi kuchukuliwa.

Alisema itakuwa udhaifu mkubwa iwapo Israel itawaruhusu Omar na Tlaib kuingia nchini humo.

Trump amedai kwamba Omar na Tlaib wanaichukia Israel na wayahudi wote, na kwamba hakuna kinachoweza kusemwa wala kufanyika kubadilisha fikra zao.

XS
SM
MD
LG