Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 11:32

Mbunge aliyetoa kauli ya ubaguzi katika bunge la Ufaransa aadhibiwa


Bunge la Ufaransa
Bunge la Ufaransa

Wabunge wengi wa Ufaransa wametaka hatua kali zichukuliwe dhidi ya mbunge wa  chama cha mrengo wa kulia zaidi  cha National Rally aliyepiga kelele akisema “rudi zako Afrika” wakati mbunge Mweusi kutoka mrengo wa kushoto akiuliza swali kuhusu uhamiaji.

Bunge la Taifa la Ufaransa lilipiga kura Ijumaa kumuadhibu mbunge wa mrengo wa kulia kumzuia kuhudhuria bunge kwa siku 15 na malipo yake kupunguzwa baada ya kupiga kelele “rudi zako Afrika” kwa mbunge mwenzake mweusi, mgogano ulioleta ghadhabu kote katika uwanja wa kisiasa.

“Ubaguzi, bila ya kujali unamlenga nani, ni kinyume cha maadili ya jamhuri ambayo inatuunganisha sote katika ukumbi huu,” rais wake Yael Braun-Pivet alisema baada ya kura kupigwa.

Maoni hayo ya Gregoire de Fournas, mbunge kutoka chama cha upinzani cha Marine Le Pen cha National Rally (RN), huku mbunge wa mrengo wa kushoto Carlos Martens Bilongo akiongea, ilizua zogo Alhamisi na kusababisha baraza kuu la bunge kusimamisha shughuli zake.

Serikali ya mrengo wa kati, na chama cha mrengo wa kushoto na kile cha mrengo wa kulia vilisema kuwa matamshi ya mbunge huyo ya kibaguzi yalikuwa hayakubaliki.

Adhabu hiyo iliyotolewa na Bunge la Taifa ni kali zaidi kutolewa kwa mujibu wa kanuni zake, ambalo linakubali wabunge wana uhuru wa kujieleza wakati wa vikao vya bunge.

Ilikuwa ni mara ya pili katika historia ya Jamhuri ya Tano ya Ufaransa, iliyoundwa na Charles de Gaulle mwaka 1958, mbunge amepewa karipio kama hilo.

De Fournas, aliondoka katika ukumbi mara baada ya upigaji kura, alitoa hisia zake kupitia Twitter akisema “mimi sina makosa kabisa… lakini naiheshimu taasisi hii, na nakubali” maamuzi yake.

XS
SM
MD
LG