Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 23:39

Ufaransa kulisaidia jeshi la Ukraine kuimarisha mifumo ya ulinzi wa anga


FILE - Kombora aina ya Caesar self-propelled howitzerst la ulinzi wa anga kutoka ardhini likiwa katika maonyesho ya biashara ya vifaa vya ulinzi na usalama June 13, 2022 , Villepinte, kaskazini ya Paris.
FILE - Kombora aina ya Caesar self-propelled howitzerst la ulinzi wa anga kutoka ardhini likiwa katika maonyesho ya biashara ya vifaa vya ulinzi na usalama June 13, 2022 , Villepinte, kaskazini ya Paris.

Ufaransa Jumapili imeahidi kupeleka mifumo ya ulinzi wa anga kuilinda miji ya Ukraine dhidi ya mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani (droni).

Ufaransa imeongeza kuwa hiyo pia ni sehemu ya programu ya kuongeza mafunzo kwa wanajeshi wa Ukraine, wakati ikijaribu kuvunja dhana iliyopo kuwa serikali ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron iko nyuma katika kulisaidia jeshi la Ukraine dhidi ya uvamizi wa Russia.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy (Kulia) alipokutana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron Feb. 8, 2022, Kyiv, Ukraine.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy (Kulia) alipokutana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron Feb. 8, 2022, Kyiv, Ukraine.

Takriban wanajeshi 2,000 wa Ukraine watashirikishwa katika vikosi vya kijeshi vya Ufaransa, na kw wiki kadhaa watapatiwa mafunzo ya kivita, mafunzo maalum katika mipango ya vita na mahitaji mengine, na vifa vitatolewa na Ufaransa, Waziri wa Ulinzi Sebastien Lecornu, alisema katika mahojiano yaliyochapishwa na gazeti la Le Parisien.

“Tunatambua ukweli kuwa vita, inasikitisha, vitaendelea,” gazeti hilo lilimnukuu waziri huyo akisema. “Kizazi kipya cha wanajeshi ni lazima kipewe mafunzo, ili waweze kudumu katika vita.”

Awali Ufaransa ilitoa mafunzo kwa wanajeshi wa Ukraine wa mizinga ili waweze kutumia makombora aina ya Caesar self-propelled howitzers waliyokuwa wametoa kwa ajili ya Ukraine.

Mafunzo hayo ya nyongeza ambayo Ufaransa inatoa hivi sasa “ni hatua muhimu,” waziri alisema. “Tunabadilisha mizani.”

Waziri huyo alisema makombora ya ulinzi wa anga aina ya Crotale ambayo Ufaransa inajitayarisha kupeleka Ukraine “yatakuwa na umuhimu wa kipekee katika kupambana na droni na mashambulizi ya makombora ya angani.”

Mfumo wa ulinzi wa Crotale.
Mfumo wa ulinzi wa Crotale.

Ufaransa inazo betri kumi na mbili, waziri huyo alisema. Lakini hakufafanua ni ngapi zitapelekwa Ukraine lakini alisema “itakuwa idadi ya kutosha kuwawezesha kulinda anga zao.”

Lengo ni kuwawezesha Ukraine kuzitumia katika kipindi cha miezi miwili, ikijumuisha muda wa mafunzo kwa wanajeshi wa Ukraine kuweza kuzitumia, waziri alisema.

Habari hii inatokana na shirika la habari la AP

XS
SM
MD
LG