Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 00:15

Rais Macron atembelea ngome ya karne ya 16 nchini Algeria


Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, wa pili kulia, akizindua mchoro unaoonyesha mji wa Oran. (AP Photo/Oleg Cetinic).
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, wa pili kulia, akizindua mchoro unaoonyesha mji wa Oran. (AP Photo/Oleg Cetinic).

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliitembelea ngome ya Santa Cruz ya karne ya 16 huko Oran, jiji la pili kwa ukubwa nchini Algeria siku ya  Jumamosi.

Kisha akapitia kwenye Disco Maghreb, duka la kihistoria na lebo ya wasanii wanaoimba muziki wa jadi nchini humo , ikiwa ni muingiliano mzuri katika safari ya Algeria iliyotawaliwa na diplomasia iliyo na utete.

Macron siku ya Ijumaa aliahidi kubadilika zaidi katika kutoa visa kwa Waalgeria baada ya mzozo mkubwa wa kidiplomasia kuzuka mwaka jana kati ya nchi hizo mbili kuhusu suala hilo.

Yeye na rais wa Algeria Abdelmajid Tebboune pia walikubaliana kuunda tume ya pamoja ya wanahistoria ambao watachunguza siku za nyuma tangu mwanzo wa ukoloni wa Ufaransa mwaka 1830 hadi uhuru wa Algeria.

Ziara yake pia ililenga kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi.

XS
SM
MD
LG