Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 00:24

Mali yaishutumu Ufaransa kukiuka anga yake

Wanajeshi wanaotawala Mali wakiwa wanalinda makao makuu yao.
Wanajeshi wanaotawala Mali wakiwa wanalinda makao makuu yao.

Mali inasema Ufaransa imekiuka anga yake kwa kupeleka silaha kwa wanamgambo wa Kiislamu katika jaribio la kuiyumbisha nchi hiyo ya Afrika Magharibi, ikiwa ni kesi ya hivi karibuni  katika msururu wa shutuma ambazo zimeashiria mwisho wa uhusiano wao wa karibu.

Katika barua kwa mkuu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa iliyoandikwa Jumatatu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali, Abdoulaye Diop, alisema anga yake imeingiliwa zaidi ya mara 50 mwaka huu, hasa na vikosi vya Ufaransa vilivyotumia ndege zisizo na rubani, helikopta za kijeshi na ndege za kivita.

Ukiukaji huu wa wazi wa anga ya Mali ulitumiwa na Ufaransa kuchukua taarifa za makundi ya kigaidi yanayoendesha shughuli zake katika Sahel na kuwapa silaha na risasi, ilisema barua hiyo.

Mali haikutoa ushahidi wowote kuonyesha kuwa Ufaransa ilitoa silaha kwa makundi ya Kiislamu. Ufaransa imetumia muongo mmoja na mabilioni ya dola kuwakomesha wanamgambo wa Kiislamu, baadhi yao wakiwa na uhusiano na al Qaeda na Islamic State, katika koloni lake la zamani.

XS
SM
MD
LG