Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 22:27

Mbunge aitaka serikali kufafanua tatizo la ugonjwa wa kupumua Tanzania


Mbunge Zacharia Isaay.
Mbunge Zacharia Isaay.

Mbunge wa Mbulu Mjini (CCM), Zacharia Isaay ameitaka Serikali ya Tanzania kuweka wazi hali aliyoiita ugonjwa wa kupumua ambao anasema unamaliza watu katika jimbo lake la Mbulu.

Isaay akizungumza kwa hisia nzito bungeni Alhamisi alisema hawezi kuzungumzia mpango uliopo mezani badala yake anaona bora ajadili hali ya wananchi wake ambao kila mara amekuwa akienda kuwazika.

"Serikali iache kigugumizi jimboni kwangu watu wanakwisha Spika, nimechoka kuzika hata leo wanazika mtoto wa diwani wakati mwingine nashindwa kukuaga Spika kwenda Mbulu naamua kutoroka," amesema Isaay.

Mbunge huyo anasema wanaofariki jimboni mwake wanakuwa na magonjwa yanayofanana na tatizo la kupumua, akiongeza kuwa anahofia kuwa msimu wa baridi jimboni kwake utaendelea kuwaumiza.

"Jana nilikwenda hospitali ya Benjamin Mkapa (Dodoma) kwa ajili ya kufanya vipimo lakini wakaniambia mitungi ya gesi imejaa, watu ni wengi sasa nimesema kama watu watanichukia basi, lakini nimesema," amesema Isaay.

Mbunge huyo ameiomba serikali kutizama njia bora ya kuboresha dawa za miti shamba ambazo ameeleza kuwa zinasaidia.

Hata hivyo amesema kwa kiasi kikubwa zinapatikana kwa gharama kubwa.

XS
SM
MD
LG