Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Agosti 17, 2022 Local time: 14:27

Tanzania yasema haina mpango wa kupokea chanjo ya COVID-19


Rais John Magufuli

Wizara ya Afya nchini Tanzania imesema Jumatatu haina mpango wa kupokea chanjo ya COVID-19 ambayo imekuwa ikiripotiwa kuwepo na kutumika katika mataifa mengine.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Doroth Gwajima amesema : ““Wizara ya Afya haina mpango wa kupokea chanjo ya Covid 19 inayoripotiwa kuwepo na kutumika katika mataifa mengine, ifahamike kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya inayo taratibu za kufuata pale inapotaka kupokea bidhaa yoyote ya afya baada ya Serikali kujiridhisha hivyo kwa nia njema kabisa ni hadi tujiridhishe na si vinginevyo.”

Akiwa katika ofisi za wizara mjini Dodoma, Dkt Gwajima amesema dhumuni la ufafanuzi huo ni juu ya maswali kadhaa ambayo amekuwa akiyapokea kutoka kwa wanahabari kuhusu kujikinga na magonjwa ya kuambukiza na yasiyo kuwa ya kuambukiza.

“Kufuatia taarifa za uwepo wa mlipuko wa pili wa ugonjwa wa corona, Covid 19 katika nchi jirani nimekuwa nikipokea maswali mengi kutoka kwa wanahabari,” amesema Dkt Gwajima.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG