Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 08, 2022 Local time: 15:18

Mazrui wa ACT-Wazalendo 'atekwa' na watu wasiojulikana


Nassor Ahmed Mazrui

Naibu Katibu Mkuu wa ACT- Wazalendo Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui anadaiwa kuchukuliwa na watu wasiojulikana baada ya gari lake kugongwa eneo la Kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU).

Inadaiwa kuwa baada ya tukio hilo watu ambao hawafahamiki walimkamata na kuondoka naye kuelekea sehemu isiyojulikana.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mjini Magharibi, Awadh Juma Haji amethibitisha tukio hilo akisema jeshi linaendelea na uchunguzi.

Kwa mujibu wa walioshuhudia na vyanzo mbalimbali vya habari, Mazrui alitekwa siku ya Jumapili eneo la Saateni wakati akielekea katika ofisi za makao makuu ya ACT-Wazalendo Vuga, Unguja.

Mazrui ni mwenyekiti wa kamati ya kampeni ya Maalim Seif Sharif Hamad, na anawania uwakilishi katika jimbo la Mwera lililopo mkoa wa Mjini Magharibi.

“Baada ya kuwasili nyumbani kwake waliligonga gari lake kutoka nyuma, ambapo wavamizi hao, wanaoshukiwa kuwa maafisa maalum wa usala, walimpiga,” taarifa ya chama hicho ilieleza, na kuongeza kwamba Abdala Ali Abdalla anayewania nafasi kwenye baraza la wawakilishi, alitekwa siku ya Jumamosi.

Wakati huohuo Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo na mgombea urais wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, amethibitisha kukamatwa kwa Naibu Katibu Mkuu Nassor Ahmed Mazrui na vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakisaidiwa na Jeshi la Polisi.

Kiongozi wa ACT-Wazalendo Zitto Kabwe katika akaunti yake ya Twitter amewataka watu waliomchukua Mazrui wamuachie mara moja.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG