Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 05:35

ZEC yasimamisha kampeni za Maalim Seif kwa siku tano


Seif Sharif Hamad
Seif Sharif Hamad

Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imemsimamisha mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, kutofanya mikutano ya kampeni za urais kwa siku tano baada ya kuonekana na kosa la uvunjifu wa maadili.

Katibu wa Kamati ya Maadili ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Khamis Issa Khamis, amesema tume ilipokea malalamiko kutoka kwa mgombea wa urais wa Chama cha Demokrasia Makini, Ameir Hassan Ameir, dhidi ya mgombea Maalim Seif ya kuhamasisha wanachama wake wakapige kura siku ya kura ya awali.

Katibu wa kamati amesema kamati ilisikiliza hoja zote na kuona kuwa mgombea Maalim Seif ametenda kosa hilo na kumpa adhabu kwa mujibu wa sheria kifungu cha 23 D za kanuni za maadili. Kamati hiyo ya maadili imetoa fursa kwa Maalim Seif kukata rufaa endapo hataridhika na maamuzi hayo.

XS
SM
MD
LG