Matukio ya 1619
#voa400 : Matukio ya 1619 : Jinsi biashara ya utumwa ilivyodhoofisha jamii za Kiafrika

“Wafanyakazi, wasomi na watu wenye ujuzi walichukuliwa kutoka hapa. Hivi leo, tunahitaji nguvu kazi hii ambayo ilikuwa na ujuzi ili Afrika iweze kusonga mbele na kufikia hali bora zaidi.” - Isilda Hurst, Mwanahistoria.
Mwaka 2019 ni maadhimisho ya miaka 400 tangu Waafrika wa kwanza kufanywa watumwa kuwasili nchi ambayo leo ni Marekani.
Kuwasili kwa meli iliyokuwa imewabeba Waafrika kutoka Angola katika koloni la Virginia, mwezi Agosti 1619, ilikuwa ni mwanzo wa kuanza biashara ya utumwa iliyodumu kwa zaidi ya miaka 200 nchini Marekani.
Mayra de Lassalette na Betty Ayoub wa VOA walisafiri hadi Angola kufahamu zaidi kuhusu chanzo kimojawapo cha biashara ya watumwa waliovushwa bahari ya Atlantic na athari zinazoendelea katika eneo hilo.
See all News Updates of the Day
#voa400 : Biashara ya Utumwa yaendelea kuwa doa kwa historia ya Marekani
Kuhusika kwa kanisa katika biashara ya utumwa jimbo la Rhode Island Marekani.
Maadhimisho ya Miaka 400 tangu watumwa wa kwanza kuwasili Marekani
Miaka 400 tangu waafrika wa kwanza waliofanywa watumwa kuwasili katika ardhi ya marekani. nchini Ghana maadhimisho haya yanaitwa “Mwaka wa Kurejea (nyumbani)” na nchi hiyo inakaribisha vizazi vya waafrika katika nchi za magharibi kwa kuwarahisishia visa na kuandaa matukio kadha kuhusu asili yao,
Mwaka huu ni 400 tangu watumwa wa kwanza kuwasili Marekani
Miaka 400 iliyopita, waafrika wa kwanza waliofanywa watumwa waliletwa marekani, wakiwasili katika koloni la kiingereza la Virginia. Kundi la kwanza lililetwa kutoka angola, baada ya kuchukuliwa na maharamia wa kiingereza kutoka meli ya kireno iliyokuwa imebeba watumwa.
#voa400 : Jinsi biashara ya utumwa ilivyoangamiza nguvu kazi Angola

Kwa karne kadhaa kuanzia mwishoni mwa miaka ya 1400, wafanyabiashara ya utumwa Wareno katika eneo ambalo ni Angola hivi leo walihusika na biashara haramu ya kusafirisha binadamu kupitia bahari ya Atlantic.
Takriban watumwa wa Kiafrika milioni 6 walitokea Angola, wengi wao walipelekwa katika makoloni ya Ureno, japokuwa baadhi yao waliishia kupelekwa Marekani Kaskazini.
Wakati baadhi ya machifu wa makabila walipata faida kwa kuuza mateka kwa wazungu waliokuwa wakifanya biashara ya utumwa, lakini wako viongozi ambao walijaribu kuwalinda watu wao.
Mayra de Lassalette na Betty Ayoub wa VOA walisafiri hadi Angola waliweza kukusanya simulizi mbalimbali juu ya mapambano makali dhidi ya biashara ya utumwa yalivyotokea. http://bit.ly/3083KTT
Wakati huohuo Ofisi ya Kumbukumbu ya Taifa Luanda, Angola inaonyesha nyaraka zilizokuwa zimehifadhiwa kwa kipindi cha miaka isiyopungua 300.
Wanahistoria wanasema kuwa Wareno waliondoka na kumbukumbu nyingi za kihistoria walipoondoka Angola baada ya nchi hiyo kupata uhuru mwaka 1975.