Dharuba ya upepo yenye kasi za zaidi ya mili 200 kwa saa imesababisha vifo vya takriban watu 50 wakiwemo watoto 20 na uharibifu mkubwa wa mali.
Dharuba kali ya upepo yasababisha maafa Oklahoma

1
John Warner anaangalia uharibifu ulofanyika katika nyumba ya rafiki yake katika uwanja wenye nyumba zenye kuhamishika wa Steelman Estates Mobile Home Park, zilizoharibiwa na dhauba karibu na Shawnee, Oklahoma, Mei 20, 2013.

2
Moto unawaka kwenye mtaa wa Tower Plaza Addition kufuatia dharuba ya upepo mjini Moore, Oklahoma, Mei 20, 2013.

3
Polisi wa mjini Moore wakifukuwa kwenye vifusi katika shule ya msingi ya Plaza Towers kufuatia dharuba kali katika mji wa Moore, Oklahoma, Mei 20, 2013.

4
Picha hii iliyochukuliwa na kituo cha televisheni cha KFOR-TV inaonesha nyumba zilizobomolewa kabisa nje ya mji wa Moore, Oklahoma, May 20, 2013.