Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 06, 2022 Local time: 03:41

Masoko ya hisa Paris na Frankfurt biashara iko juu wakati la London limefungwa


Watu wykiwa katika stesheni ya roli Yokohama, jimbo la Kanagawa karibu na Tokyo, Alhamisi, Mei 21. Amri ya dharura inatarajiwa kumalizika mwisho wa mwezi Mei, japokuwa hapakuwa na masharti magumu ya kutotoka nje wakati huo wa amri ya dharura.

Masoko ya fedha ya Ulaya yanafanya biashara kwa thamani ya juu Jumatatu.Markets in Paris and Frankfurt Trading Higher with London Closed

Kipimo cha hisa cha Paris CAC-40 kiko juu kwa asilimia 1, wakati DAX huko Frankfurt kikiwa kimeongezeka kwa asilimia 1.5. Kipimo cha hisa cha Uingereza FTSE kimefungwa kwa sababu ya sikukuu hii leo.

Kipimo cha hisa cha Tokyo Nikkei kilifunga biashara kikiwa asilimia 1.7 juu baada ya taarifa kwamba serikali ilikuwa tayari kuondoa hali ya dharura mjini Tokyo.

Wakati huohuo kipimo cha hisa cha Hong Kong, Hang Seng kilimaliza biashara yake kikiwa asilimia 0.1 juu zaidi baada ya msukosuko wa siku nzima wakati maandamano mapya yalipoanza katika mtaa wa biashara na fedha.

Maandamano hayo yanatokana na kupendekezwa kwa sheria mpya ya usalama wa taifa inayoshawishiwa na China ambapo wanaoikosoa wanasema italeta ukomo kwa hali ya uhuru wa kujitawala ya mji huo.

Kipimo cha hisa cha Shanghai kilimaliza biashara kikiwa juu kwa asilimia 0.15, wakati kipimo cha hisa cha Sydney S&P /ASX kilifunga biashara kikiwa juu kwa asilimia 2.1. Kipimo cha Seoul KOSPI kiko juu kwa asilimia 1.2, wakati kile Taiwan TSEC kilifunga biashara siku hii kikiwa chini kwa asilimia 0.5%.

Katika soko la biashara ya mafuta ghafi, mafuta ya Marekani yanauzwa kwa dola 33.49 kwa pipa, hivyo ikiwa imepanda kwa karibu asilimia 0.7, wakati soko la kimataifa la mafuta ghafi ya Brent, limebakia katika bei ya dola 35.11 kwa pipa.

Miamala yote ya masoko yote matatu ya fedha ya Marekani imefungwa kwa sababu ya kuadhimisha sikukuu ya kumbukumbu ya mashujaa Marekani.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG