Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 06:20

Marekani yataka Russia iondolewe kutoka Baraza la Haki za Binadamu


FILE PHOTO: Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa balozi Linda Thomas Greenfield., Picha na REUTERS/Brendan McDermid/File Photo
FILE PHOTO: Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa balozi Linda Thomas Greenfield., Picha na REUTERS/Brendan McDermid/File Photo

Marekani italiomba Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa- UNGA kuiondoa Russia katika Baraza la haki za binadamu, amesema hayo balozi wa Marekani katika umoja huo.

“Ushiriki wa Russia katika baraza la haki za binadamu ni kituko. Si sahihi ndio maana tunaamini wakati umefika kwa baraza kuu la umoja wa mataifa kupiga kura kuwaondoa,” amesema balozi Linda Thomas Greenfield.

Ukraine imeishutumu Russia kwa kufanya mauaji ya makusudi, baada ya miili ya takriban watu 20 waliovaa nguo za kiraia kukutwa kwenye mitaa katika mji.

Inasemekana mamia ya miili iligundulika katika mitaa ya miji nje ya Kyiv kufuatia kujiondoa kwa wanajeshi wa Russia katika eneo hilo kwa mujibu wa maafisa wa Ukraine.

Hata hivyo Russia imekanusha kufanya mauaji yoyote. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy ameutembelea mji wa Bucha, huku ushahidi wa mauaji unazidi kuibuka.

Alikagua barabara ambayo wanajeshi wa Russia walivamiwa, na kuzungumza na wakaazi wa ndani.

Amerejea kusema kuwa Russia imefanya uhalifu wa vita na mauaji ya kimbari ndani ya Ukraine. Watu zaidi ya milioni mbili wamekimbia Ukraine kwenda Poland tangu vita vilipoanza , walinzi wa mpakani wa Poland wamesema.

XS
SM
MD
LG