Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 04, 2024 Local time: 00:36

Zelenskyy aomba msaada zaidi wa kijeshi kutoka NATO

Waziri Mkuu wa Japan, Fumio Kishida, kushoto, Rais wa Marekani Joe Biden, wa pili kushoto na Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz, mbele kulia, wakizungumza na Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg katika mkutano wa NATO, Alhamisi March 24, 2022. (Henry Nicholls/Pool via AP)

Akihutubia viongozi hao kwa njia ya video kutoka Kyiv, Zelensky amesema kwamba Ukraine imeonyesha uwezo wake wa kijeshi na kwamba jukumu kwa sasa ni NATO kuonyesha kwamba kwa hakika ni muungano wenye nguvu sana wa kijeshi duniani.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amehutubia muungano wa NATO na kuomba msaada zaidi wa kijeshi ili aweze kupambana vilivyo na wanajeshi wa Russia.

Akihutubia viongozi hao kwa njia ya video kutoka Kyiv, Zelensky amesema kwamba Ukraine imeonyesha uwezo wake wa kijeshi na kwamba jukumu kwa sasa ni NATO kuonyesha kwamba kwa hakika ni muungano wenye nguvu sana wa kijeshi duniani.

Rais wa Ukraine amesema kuwa: "Mnamo Februari 24, niliwahutubia na nikawasilisha ujumbe wangu wa kuomba anga yetu ifungwe kwa safari za ndege. Kwa namna yoyote, tunastahili kulinda watu wetu kutokana na mashambulizi ya mabomu na makombora ya Russia.

Hatukupata jawabu muafaka. Ukraine haina mitambo ya kuzima makombora na ina ndege ndogo za kijeshi ikilinganishwa na Russia. Kwa hivyo, nguvu walizo nazo angani zinatuzidi na ni kama kutumia silaha zenye uwezo wa kufanya uharibifu mkubwa."

Rais wa Marekani Joe Biden na viongozi wengine wa dunia wanakutana wakati Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg akionya ni lazima muungano huo uimarishe ulinzi wake ili kukabiliana na uvamizi wa Russia nchini Ukraine, pamoja na kujibu tishio kubwa la usalama barani Ulaya.

Stoltenberg amesema hayo wakati akifungua kikao cha NATO, kinachoangazia namna ya kuongeza shinikizo dhidi ya rais wa Russia Vladimir Putin, kutokana na uvamizi wake Ukraine, pamoja na kukabiliana na changamoto za kiusalama na kiuchumi barani Ulaya na duniani.

Wakati huo huo, viongozi wa Kremlin wamesema kwamba hatua ya kuwafukuza wanadiplomasia wa Marekani ilikuwa ya lazima baada ya Washington kuwafukuza wanadiplomasia 12 wa Russia kutoka Umoja wa Mataifa, New York, kutokana na sababu za kiusalama.

Ubalozi wa Marekani mjini Moscow umesema kwamba umepokea orodha ya wanadiplomasia ambao serikali ya Putin imesema kwamba hawaruhusiwi kuwa nchini humo, vyombo vya habari vya Russia vikisema kwamba ilikuwa hatua ya kujibu hatua iliyochukuliwa na Marekani katika Umoja wa Mataifa.

Nchini Ukraine, wizara ya ulinzi imesema kwamba wanajeshi wake wamepiga na kuharibu meli ya Russia katika bandari ya Berdiansk katika Black sea.

Na rais wa shirika la kimataifa la msalaba mwekundu amesema kwamba amefanya mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergrei Lavrov kuhusiana na umuhimu wa kuwalinda raia katika vita vinavyoendelea Ukraine.

XS
SM
MD
LG