Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 14:34

Viongozi wenye nguvu duniani wakubaliana kutolegeza msimamo dhidi ya Russia


Mwanajeshi wa Ukrain akiwa katika vita mjini Kyiv kutokana na uvamizi wa RUssia nchini humo March 29, 2022. Picha AP
Mwanajeshi wa Ukrain akiwa katika vita mjini Kyiv kutokana na uvamizi wa RUssia nchini humo March 29, 2022. Picha AP

Viongozi wa Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Italy, wametoa wito kwa mataifa ya magharibi kutolegeza msimamo wake dhidi ya Russia.

Hii ni baada ya Moscow kuonyesha dalili za kupunguza mashambulizi dhidi ya Ukraine katika miji ya Kyiv na miji mingine.

Waziri wa mambo ya nje wwa Uturuki Mevlut Cavusoglu, ametangaza kwamba katika mazungumzo ya amani yanayoendelea Istanbul, wajumbe wa Russia na Ukraine wamekubaliana kuhusu badhi ya mambo.

Akizungumza na waandishi wa habari mda mfupi baada ya mazungumzo yake ya simu na viongozi wa nchi nne za ulaya ambazo ni washirika wakubwa wa Marekani, rais Joe Biden amesema kwamba wanasubiri kuona kama makubaliano yatafikiwa katika mazungumzo kati ya Russia na Ukraine.

Biden amesema kwamba inaonekana kwamba wajumbe katika mazungumzo hayo wamefikia makubaliano kuhusu baadhi ya mambo, lakini kinachosubiriwa ni kuona matokeo ya mazungumzo hayo.

"kwa sasa, tutaendelea kutekeleza vikwazo vikali, tutaendelea kutoa msaada wa kijeshi kwa Ukraine ili wajilinde wenyewe, na tutaendelea kufuatilia kwa karibu sana kinachoendelea.” Amesema rais wa Marekani Joe Biden.

White house yaelezea yaliyozungumziwa katika mkutano

White House imesema kwamba viongozi hao watano wamekubaliana kutekeleza vikwazo vikali vya kiuchumi dhidi ya Moscow kutokana na uvamizi wake Ukraine.

Msemaji wa Pentagon John Kirby, amesema kwamba wanajeshi wa Russia wameanza kundoka mji mkuu wa Ukraine, Kyivm na hawapo karibu na mji huo, baada ya Moscow kusema kwamba itapunguza mashambulizi ya kijeshi karibu na mji huo.

"Haina maana kwamba tishio dhidi ya Ukraine limemalizika. Russia imeshindwa kutimiza lengo lake la kuteka Ukraine lakini wanaweza kutekeleza uharibifu na dhuluma kubwa dhidi ya nchi hiyo, ikiwemo Kyiv. Tunaona kwamba hata leo, wametekeleza mashambulizi ya angani dhidi ya mji mkuu.”

Moscow yazungumzia kuhusu mapendekezo ya Ukraine

Mjini Moscow, msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amesema kwamba ni hatua nzuri kwamba Ukraine imeasilisha mapendekezo katika mazungumzo ya Istanbul, lakini pia akaongezea kwamba hakuna makubaliano yamepatikana.

"Hii ni hatua nzuri. Kwa sasa, hatuwezi kusema kwamba kuna mafanikio yoyote yamepatikana. Bado tuna kazi chungu nzima ya kufanya.” Amesema Dmitry Peskov.

Russia imetangaza kwamba itapunguza mashambulizi yake ya kijeshi karibu na mji mkuu wa Ukraine.

Ukraine yasema wanajeshi wa Russia wanajipanga upya

Mkuu wa jeshi la Ukraine hata hivyo amesema kwamba wanajeshi wa Russia wanajikusanya ili kushambulia sehemu ya mashariki mwa Ukraine.

Wanajeshi wa Ukraine walio sehemu za vijijini za Brovary, karibu na Kyiv, wanasema kwamba wameona dalili zinazoonyesha kwamba wanajeshi wa Russia hawafanyi shughuli nyingi kama ilivyokuwa awali.

Idadi ya wakimbizi yaongezeka

Shirika la kuwahudhumia wakimbizi la umoja wa Mataifa UNHCR, limesema kwamba zaidi ya watu milioni 4 wamekimbia Ukraine, milioni 2.3 kati yao wakiwa wamekimbilia Poland, kufuatia uvamizi wa Russia, ikiwa ni wimbi kubwa la wakimbizi kuwahi kutokea Ulaya tangu vita vya pili vya dunia.

Afisa wa ngazi ya juu wa UNHCR nchini Poland, Alex Mundt, ameonya kwamba idadi ya wakimbizi huenda kikaongezeka zaidi.

"Kufikia leo, jumla ya watu milioni 4 wamekimbia Ukraine. Nadhani ni hali ya kusikitisha kabisa. Hii ina maanda kwamba katika mda wa mwezi mmoja, watu milioni 4 wamekimbia nyumbani kwao na familia kuvurugwa pamoja na jamii zao. Hii ndio idadi kubwa ya wakimbizi kuwahi kutokea katika siku za hivi karibuni.” Amesema Mundt.

Wafanyakazi wa kutoa msaada wamesema kwamba idadi ya wakimbizi wanaovuka mpaka na kuingia Poland imepungua katika siku za hivi karibuni, huku watu wengi wakisubiri kujua kinachotokea katika mazungumzo ya amani yanayoendelea.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG