Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:47

Marekani yataja mafanikio lakini yatahadharisha mkataba unaweza kufa kabla ya Iran kuutekeleza


Naibu Katibu Mkuu wa EEAS inayoshughulikia Huduma za Nje za Ulaya, Enrique Mora na Mkuu wa Mazungumzo ya Nyuklia wa Iran Ali Bagheri Kani na wajumbe waKisubiri kuanza mkutano wa JCPOA, Vienna, Austria Disemba 17, 2021EU Delegation in Vienna/EEAS/Handout via REUTERS
Naibu Katibu Mkuu wa EEAS inayoshughulikia Huduma za Nje za Ulaya, Enrique Mora na Mkuu wa Mazungumzo ya Nyuklia wa Iran Ali Bagheri Kani na wajumbe waKisubiri kuanza mkutano wa JCPOA, Vienna, Austria Disemba 17, 2021EU Delegation in Vienna/EEAS/Handout via REUTERS

Marekani inasema mazungumzo yake yasiyokuwa ya moja kwa moja na Iran ya kufufua makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015 yamepiga hatua kiasi katika duru ya karibuni iliyomalizika Ijumaa.

Lakini pia inasema kazi kubwa bado inatakiwa kufanywa ili kuzuia kile kilichosalia katika mkataba huo kati ya Tehran na mataifa yenye nguvu kabla ya kuvunjika haraka.

Katika maelezo yake kwa njia ya simu kwa waandishi wa habari, afisa wa ngazi ya juu wa Wizara ya Mambo ya Nje ameelezea mifano miwili ya hatua ya kiasi iliyopigwa katika mazungumzo hayo ya Vienna ikiihusisha Marekani, Iran na mataifa matano yenye nguvu duniani wakiwa ni wasuluhishi kati ya pande hizo mbili.

La kwanza yalikuwa ni makubaliano ambayo Iran imeyakubali Jumatano kuliruhusu shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomic kuweka kamera ambazo zitawaruhusu wakaguzi wa Umoja wa Mataifa kuangalia kiwanda cha nyuklia cha Iran kinachotengeneza mabomba ya nyuklia katika hatua ya juu katika mji wa Karaj.

Kamera hizo ziliharibiwa mwezi Juni katika kile Iran ilichokiita ni kitendo cha njama ilichofanywa mahasimu wao wa kieneo Israel, jambo ambalo halijathbitishwa wala kukanusha kuhusika kwake.

Mfano wa pili ulioelezewa na maafisa wa Marekani ni kile wanachokubaliana pande zote Marekani na Iran ni maandishi ambayo yatatumika kama msingi wa mashauriano juu ya sehemu zipi za programu ya nyuklia zinaweza kusitishwa kwa ajili ya kuondoa vikwazo vya Marekani dhidi ya Tehran.

Lakini maafisa wa Marekani wameonya dhidi ya kuwa na shauku kubwa juu ya maandishi hayo.

Afisa wa Marekani pia amesema hatua za karibuni za Iran katika programu yake ya nyuklia ambazo nchi za Magharibi zina wasiwasi wanaweza kutengeneza silaha ni umuhimu sana kwa Tehran kurejea katika utekelezaji uliowekwa katika programu hiyo uliokubaliwa siku za nyuma chini ya makubaliano ya mwaka 2015, yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Hatua ya Pamoja (JCPOA).

“Tumepata mafanikio kadhaa, lakini … kwa kasi ambayo haitatosheleza kufika pale tunapotaka kufika kabla ya hatua ya Iran kufikia silaha ya nyuklia hazijaigeuza JCPOA ni mfu ambaye hawezi kufufuliwa tena,” afisa huyo amesema.

Iran ambayo imesema shughuli zake za nyuklia ni kwa malengo ya amani, imekuwa ikivuka masharti yaliyowekewa katika harakati zake za nyuklia tangu mwaka 2019 ikiwa ni majibu kwa hatua ya Marekani kujitoa katika JCPOA mwaka moja kabla.

Rais wa zamani Donald Trump
Rais wa zamani Donald Trump

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump alijitoa katika JCPOA na yeye peke yake akazidisha vikwazo dhidi ya Iran, akisema ilikuwa njia bora kuishinikiza Tehran kuacha vitendo vya udanganyifu.

Mrithi wa Trump, Rais Joe Biden, amesema kurejea kwa Marekani katika JCPOA ni njia bora kuizuia Iran kutengeneza silaha katika program yake ya nyuklia, iwapo tu Tehran inarejea kuheshimu makubaliano.

Rais Joe Biden
Rais Joe Biden

Mapema Ijumaa, Ali Bagheri Kani, mpatanishi mkuu wa masuala ya nyuklia wa Iran na naibu waziri wa mambo ya nje, alituma ujumbe wa Twitter akisema “hatua nzuri” imefikiwa hapa Vienna katika duru ya saba ya mazungumzo ya Iran yasiyokuwa ya moja kwa moja na Marekani, kufuatia duru sita zilizopita zilizofanyika kuanzia Aprili hadi Juni.

XS
SM
MD
LG