Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 27, 2023 Local time: 04:03

Naftali Bennett alalamikia Iran mbele ya mkutano wa UN


Waziri mkuu npya wa Israel Naftali Bennett

Waziri mkuu mpya wa Israel Naftali Bennett Jumatatu ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua ya pamoja dhidi ya Iran wakati akidai kwamba Tehran imeendelea na program ya utengenezaji wa nyuklia, akisema kwamba iwapo hilo halitafanyika, basi yeye atachukua hatua mwenyewe.

Wakati wa hotuba yake ya kwanza mbele ya baraza kuu la Umoja wa Mataifa,Bennett hakutaja mgogoro wa muda mrefu kati ya Israel na Palestina, na badala yake alionekana kulaumu Iran kama adui mkubwa kwenye usalama wa kimataifa.“Program ya nyuklia ya Iran imefika kilele, nao ustahimilivu wetu pia umefika mwisho,” Ameongeza Bennett.

Baada ya kufanyika kwa uchaguzi usiokamilika kwa miaka miwili, Bennett hatimaye alichukua nafasi ya waziri mkuu wa muda mrefu Benjamin Netanyahu mwezi Juni baada ya kuunda serikali ya muungano wa vyama tofauti vya kisiasa, suala ambalo llilibadili siasa za Israel

Bennett aliongeza kusema kwamba ni dhahiri kwa kila mwenye macho kwamba nia ya Iran ni kuchukua udhibiti wa kieneo kwa kutumia uwezo wake wa ki nyuklia. Kiongozi huyo amemtaja rais mpya wa Iran Ebrahim Rais kama mchinjaji wa Tehran kutokana na jukumu lake la awali la kukanadamiza wakosoaji pamoja na kutoa ufadhili kwa maadui wa Israel.Facebook Forum

XS
SM
MD
LG