Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 18:09

Kundi la G7 linasema muda unakwisha kwa Iran kukubali makubaliano yake ya nyuklia


Mawaziri kutoka mataifa ya G7 kwenye mkutano wa Uingereza. Dec. 12, 2021.
Mawaziri kutoka mataifa ya G7 kwenye mkutano wa Uingereza. Dec. 12, 2021.

Mawaziri wa mambo ya nje kutoka mataifa tajiri sana duniani walifanya mkutano wa siku mbili mjini Liverpool, kaskazini-magharibi mwa Uingereza, wakitaka kuwasilisha msimamo thabiti wa pamoja  dhidi ya vitisho ulimwenguni

Kundi la G7 leo Jumapili lilisema muda unazidi kuyoyoma kwa Iran kukubali makubaliano ya kuzuia malengo yake ya nyuklia na kuionya Russia kuhusu madhara ya kuivamia Ukraine.

Mawaziri wa mambo ya nje kutoka mataifa tajiri sana duniani walifanya mkutano wa siku mbili mjini Liverpool, kaskazini-magharibi mwa Uingereza, wakitaka kuwasilisha msimamo thabiti wa pamoja dhidi ya vitisho ulimwenguni.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, Liz Truss
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, Liz Truss

Kuhusu Iran, mwenyeji wa G7 Uingereza ilisema mazungumzo yaliyoanza tena mjini Vienna yalikuwa nafasi ya mwisho ya Jamhuri ya Kiislam ya kufika kwenye meza ya mashauriano na azimio zito. Bado kuna wakati kwa Iran kuja na kuukubali mkataba huu Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Liz Truss aliuambia mkutano wa waandishi wa habari wakati mazungumzo yalipokamilika.

Mazungumzo yalianza tena Alhamis iliyopita kujaribu kufufua makubaliano yam waka 2015 kati ya Iran na mataifa yenye nguvu duniani, ambapo Marekani ilijiondoa wakati wa utawala Rais wa wakati huo Donald Trump mwaka 2018.

XS
SM
MD
LG