Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 29, 2022 Local time: 16:59

Marekani na Israel zinasema zinajiondoa kutoka UNESCO


Shirika la elimu na sayansi la Umoja wa Mataifa-UNESCO

Marekani inasema inajiondoa kutoka shirika la elimu na sayansi la Umoja wa Mataifa- UNESCO ikiishutumu taasisi hiyo kwa uwonevu dhidi ya Israel. Wizara ya mambo ya nje Marekani ilithibitisha kwamba Marekani itajiondowa rasmi Disemba 31 mwaka 2018.

Saa kadhaa baadae Israel ilitangaza kwamba pia itajitoa kutoka uanachama wa taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa-UNESCO. Taarifa kutoka ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ilisema Waziri Mkuu aliielekeza wizara ya mambo ya nje kuandaa barua ya Israel kujitoa kutoka taasisi hiyo ikiungana na Marekani.

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu.
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu.

Bwana Netanyahu aliukaribisha uamuzi uliofanywa na Rais wa Marekani Donald Trump wa kujitoa kutoka UNESCO. Kwa upande wake UNESCO ilijibu kwa masikitiko uamuzi huo uliofanywa na Marekani.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG