Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 16:49

Je, nini hatma ya ushindani wa China na Marekani katika sekta ya teknolojia ya mawasiliano Barani Afrika?


Rais wa Marekani alipokuwa akijadiliana na Rais wa China kuhusu uvamizi wa Russia huko Ukraine.
Rais wa Marekani alipokuwa akijadiliana na Rais wa China kuhusu uvamizi wa Russia huko Ukraine.

Katika miaka ya karibuni Afrika, imekuwa ni sehemu muhimu ambayo China na Marekani, mataifa mawili duniani yenye uchumi mkubwa sana, yanashindana kupata ushawishi katika sekta muhimu: mawasiliano.

Katika miaka ya karibuni Afrika, imekuwa ni sehemu muhimu ambayo China na Marekani, mataifa mawili duniani yenye uchumi mkubwa sana, yanashindana kupata ushawishi katika sekta muhimu: mawasiliano.

Wiki hii, Ethiopia ilisherehekea kuzinduliwa rasmi kwa mtandao wa 5G na kampuni kubwa ya mawasiliano ya China, Huawei mjini Addis Ababa.

Kabla ya hapo, ziara yake katika bara hilo hivi karibuni, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Wendy Sherman aliitembelea kampuni ya Marekani ya simu za mkononi Africell nchini Angola, ambako kampuni hiyo ina takriban wateja milioni 2 tangu kuanzishwa kwake kiasi cha mwezi mmoja uliopita.

Leo hii mjini Luanda, niliitembelea kampunoi ya AfricellAo, ina teknolojia ya kisasa, imepanuafursa ya upatikanaji wa mtandao wa 5G nchiniAngola kwa kutumia vifaa vya uhakika,” aliandikanaibu Waziri wa Mambo ya Nje katika tweet yake. https://twitter.com/DeputySecState/status/1522239697291911172 ]].

Akiulizwa katika mikutano kadhaa ya wana habari iwapo tweet yake haikuwa inawalenga Huawei – ambayo tayari ina uwepo mkubwa sana barani Afrika lakini imewekewa vikwazo na Marekani mwaka 2019 na rais wa zamani Donald Trump – Sherman hakuna nashaka.

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump

“Siyo kuhusu kuwakosoa Huawei. Tumekuwawazi. Tunaamini kwamba wakati nchizinapoichagua Huawei, wanachia mamlaka yao,” alisema. “wanakabidhi data zao kwa nchinyingine. Huenda wakajikuta wakiingiza uwezowa kipelelezi ndani ya nchi yao bila ya wao kujuaulikuwepo.”

Washington kwa muda mrefu imeelezea wasiwasi wake kwamba Beijing inajaribu kutawala mitandao na kuna uwezekano wa kuitumia kwa ujasusi, wakati Huawei imerejea kukanusha shutuma hizo.

“Kwa hiyo, tumekuwa wazi kuhusu wasi wasi wetu kwa Huawei, na tuna furaha kusema kwamba Africell inaweza kuwapatia watu wa Angola huduma salama, nyenzo muafaka katika mikono yao na kuifikia dunia,” Sherman alisema.

Maoni ya naibu Waziri yameongeza hasira huko Beijing, ambako yalipata majibu makali kutoka kwa msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Zhao Lijian.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Zhao Lijian
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Zhao Lijian

“Makampubni ya China ikiwa pamoja na Huawei yamekuwa na ushirikiano wenye tija kwa pande zote huku nchi nyingi barani Afrika na dunia kwa jumla zimechangia katika kuboresha na maendeleo ya nchi katika miundombinu yamawasiliano, ya hali ya juu, bora, salama na huduma ambazo wanaweza kuzimudu watu katika eneo husika na kupata msaada mkubwa,” alisema kwenye vyombo vya habari vya China.

“Hakuna hata kesi moja ya ajali ya mtandao, upelelezi au kusikiliza mawasiliano katika kipindi cha ushirikiano,” aliongeza, akiendelea kushutumu kuwa Marekani kwa muda mrefu imehusika na harakati kama hizo za kipelelezi.

Zhao alielezea kwamba ni juu ya serikali za Kiafrika kuamua nani wanataka kushirikiana naye.

Nchini Angola, kampuni tayari ina uwepo mkubwa sana, huku kampuni ya simu ya Unitelikiunganishwa na Huawei, ambayo pia inajengavituo viwili vya teknolojia, vyenye thamani ya dolamilioni 60, nchini humo ili kuendeleza uchumi wakidigitali.

Wateja na wafanyakazi wakiwa katika duka la Huawei katika eneo la biashara la Sandton City, Sandton, Afrika Kusini, Feb. 16, 2022.
Wateja na wafanyakazi wakiwa katika duka la Huawei katika eneo la biashara la Sandton City, Sandton, Afrika Kusini, Feb. 16, 2022.

Huawei inapatikana sana Afrika Kusini, mtummoja kati ya watano aliyezungumza na VOA katika duka moja alikuwa anafahamu kuhusumzozo uliopo juu ya huduma ya 5G.

Cheris Fourie, mshauri wa mauzo katika duka moja la simu za mkononi mjini Cape Town katika eneo la maduka la Blue Root, alisema simu za Huawei si maarufu sana hivi sasa, siyo kwa sababu ya harakati zozote mbaya za kampuni hiyo, lakini kwa sababu huduma za Google hazimotena kwenye simu hizo. Google haipo kwa sababu ya marufuku ya Marekani kwa Huawei.

David Devillieras, ambaye amekaa kwenye mgahawa mmoja katika eneo hilo la maduka ambaye anatumia simu ya Samsung, ameiambiaVOA kuwa hajawahi kusikia uwezekano wa Huawei kuhusika na ujasusi wa aina yoyote. Aliongeza kwamba hatanunua simu ya Huawei baada ya kusikia hayo.

“Sita kwenda huko kabisa, hata kwa dakika moja. Sitanunua simu ya kichina,” alisema.

Mnunuzi mmoja, Steve Elliot-Jones, alisema “hataamini chochote ambacho kinatoka China,” lakini anadhani pia kuna nchi nyingine ambazo zinatumia mitandao ya simu kufanya upelelezi.

“Haitanishangaza kama teknolojia ya makampuni ikiwa ni pamoja na serikali au kwingineko kote kuhusu hilo…. Siwezi kusema nani hana hatia. Nadhani kwa hakika wote wanauza habari nakujitengenezea pesa pembeni na kukanushakama hilo likijitokeza hadharani.”

XS
SM
MD
LG