Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 15, 2024 Local time: 12:47

Mkutano wa Marekani na China utaangaza masuala ya hali ya hewa na waandishi wa habari


Mkutano wa Rais wa Marekani Joe Biden na Rais wa China Xi JInping kupitia mitandao Jumatatu, Nov. 15, 2021. (AP Photo/Susan Walsh)
Mkutano wa Rais wa Marekani Joe Biden na Rais wa China Xi JInping kupitia mitandao Jumatatu, Nov. 15, 2021. (AP Photo/Susan Walsh)

China na Marekani zitatumia fursa nadra ya mkutano wa uongozi mapema wiki hii kufikia malengo yao katika kushughulikia masuala ya hali ya hewa na majadiliano ya waandishi wa habari.

Lakini itayaacha pembeni masuala kama vile kuongezeka kwa uwepo wa majeshi katika eneo la bahari ya Pacific Asia mpaka mahusiano yatakapo boreka, wachambuzi wanaamini hilo.

Rais wa Marekani Joe Biden alikutana na kiongozi mwenzake wa China Xi Jinping Jumatatu katika mkutano wa njia ya video.

Xi alitetea uhuru wa China na kupendekeza ushirikiano wakati Biden akihimiza kupunguza hatari ya mgogoro na kumtaka Xi kuheshimu haki za binadamu na hatma ya Taiwan.

“Nafikiri inafungua hali ya ushirikiano katika maeneo mepesi lakini siyo katika masuala mazito ya kiusalama,” amesema Carl Thayer, Profesa anaye heshimika mtaalam wa masuala ya Asia kutoka Chuo Kikuu cha New South Wales huko Australia.

Nchi hizo mbili ni mahasimu tangu kipindi cha Vita Baridi, huku maamuzi yao yakionyesha majigambo au kutoa changamoto kwa serikali nyingine kutoka kote Asia hadi katika bara la Amerika.

Serikali ya Marekani inaiona China kama mpinzani wa kimkakati wakati Beijing ikitafuta kuongeza nguvu zake za kijeshi na ushawishi wa kiuchumi katika eneo la pwani.

Pande hizo mbili zilikuw ana mabishano ya kibiashara – huku bidhaa za dola bilioni 550 zikiwa ni kiini cha kulipiwa ushuru wa juu sasa kuliko ilivyokuwa mwaka 2018 – na juu ya siri za kiteknolojia pamoja na maeneo nyeti ya kijeshi.

Mafahari hao wote wawili wamepeleka manuari za kivita kwenye mlango wa vagharu wa Taiwan na bahari ya South China.

Vyombo vya majini vinavyomilikiwa na China vikiwa katika Bahari ya South China.
Vyombo vya majini vinavyomilikiwa na China vikiwa katika Bahari ya South China.

Kila upande imekubali kulegeza masharti ya kutoa visa kwa waandishi wa habari wa kila upande, na kuondoa vikwazo vilivyowekwa mwaka jana.

Litakalofuatia ni makubaliano ya kikundi cha ushirikiano cha China na Marekani katika biashara na mazingira, amesema Yun Sun, mkurugenzi mwenza wa programu ya Asia ya Mashariki huko katika Kituo cha Stimson, Washington.

Nchi hizo mbili zimesaini azimio la pamoja Novemba 10 katika mkutano wa COP26 wa Hali ya Hewa Duniani linalozikata nchi hizo kuchukua hatua kudhibiti kuongezeka kwa joto duniani katika muongo ujao.

Katika masuala nyeti zaidi, Marekani imeweka mpango ambayo huenda ikaikasirisha China, wachambuzi wanasema.

Biden atazungumza katika mkutano wa demokrasia ya Ulimwenguni Disemba 9 na 10 kwa njia ya mtandao ambapo viongozi kutoka nchi 100 watahudhuria.

Mkutano huo umelenga kuhamasisha demokrasia dhidi ya utawala wa kidikteta, itakuwa ni pigo kwa China.

Huko Asia, Washington inaendeleza mkakati wa kiuchumi wa nchi za Indo-Pacific wiki hii huku zikiwepo ziara kadhaa za Waziri wa Biashara wa Marekani Gina Raimondo kuelekea Japan, Malaysia na Singapore.

Tovuti ya habari ya Global Times inayofuatiliwa na serikali ya China imeutia ila mkakati huo kuwa ni mkongwe kwa zaidi ya miaka 10 na hauna nguzo za kiuchumi.

Katika upande wa kijeshi, Marekani imemaliza zoezi la kwanza la kukabiliana na meli aina ya Submarine, huko Bahari ya South China ikishirikiana na Japan na kufanya mazungumzo na Ufilipino juu ya eneo hilo la majini, ambapo Beijing ina nguvu zaidi za kijeshi katika eneo kuliko nchi nyingine huru ikiwemo Manila.

Biden anaweza kutangaza kususia kidiplomasia michezo ya Olimpiki ya Wakati wa Majira ya Baridi yaliyopangwa kufanyika Beijing mwaka ujao, Sun amesema, akinukuu maoni yaliyokuwa katika Gazeti la Washington Post la Novemba 16.

XS
SM
MD
LG