Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 28, 2023 Local time: 22:08

Biden na Xi watarijiwa kufanya mazungumzo ya kwanza kwa mtandao


Rais Joe Biden (Kulia) na Rais Xi Jinping
Rais Joe Biden (Kulia) na Rais Xi Jinping

Mazungumzo ya kwanza kati ya Marais Joe Biden wa Marekani na Xi Jinping wa China yanatarajiwa kafanyika kupitia mawasiliano ya mtandao Aprili 22, wakati Biden atapoongoza mkutano wa viongozi wa dunia juu ya mabadiliko ya hali ya hewa mjini Washington.

Mkutano huo unalengo la kuwaleta pamoja vongozi wa dunia kujadli mabadiliko ya hali ya hewa, suala ambalo Biden amesema ni kiungo muhimu cha sera za kigeni na usalama wa kitafa wa Marekani.

Maafisa wa Marekani wamesema China ndio mchafuzi mkuu wa gesi ya carbon duniani ikizalisha asilimia 30 ya gesi ya mkaa.

Marekani ni nchi ya pili inayozalisha aslimia 15 na nchi hizi mbili zimetangaza nia ya kupunguza kabisa utowaji wa gesi hiyo kufikia 2050.

Kwa upande mwengine mkutano wa kwanza wa ana kwa ana wa maafisa wa vyeo vya juu wa Marekani na China utafanyika kesho Alhamisi mjini Anchorage Alaska kati ya Mawaziri wa Mambo ya NVje Antony Blinken wa Marekani na Wang Yi wa China.

XS
SM
MD
LG