Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 18:30

Wajasiria mali Kenya wanasema wanapoteza soko la bidhaa zao  kutokana na  bidhaa za China


Mazungumzo kati ya Rais Kenyatta na ujumbe wa China ukiongozwa na waziri mkuu wa China Li Keqiang huko Beijing China.Agosti 20,2013.(AP Photo/How Hwee Young).
Mazungumzo kati ya Rais Kenyatta na ujumbe wa China ukiongozwa na waziri mkuu wa China Li Keqiang huko Beijing China.Agosti 20,2013.(AP Photo/How Hwee Young).

Wajasiria mali Kenya wanasema wanapoteza soko la bidhaa zao  kutokana na  bidhaa za China. Kwa mujibu wa wafanyabiashara hao, ubora wa juu na bei za chini kwa bidhaa kutoka China zinawaweka katika hali isiyo nzuri kibiashara.

Wajasiria mali Kenya wanasema wanapoteza soko la bidhaa zao kutokana na bidhaa za China. Kwa mujibu wa wafanyabiashara hao, ubora wa juu na bei za chini kwa bidhaa kutoka China zinawaweka katika hali isiyo nzuri kibiashara.

Kundi la Jua kali, maarufu sana nchini Kenya kwa kazi zake za utengenezaji bidhaa au nguo, limekuwa likiwa ni mhimili wa kimaisha wa zaidi ya wasanii 7,000 ambao wanafanya shughuli zao katika soko la wazi katika mji mkuu wa Kenya kwa miongo mingi.

Njoroge Macharia amekuwa akitengeneza majiko yanayotumia mkaa, ambayo ni maarufu sana, kwa miongo minne. Anasema uagizaji bidhaa kutoka China umeifanya biashara yake kuwa katika hali ya mashaka. Majiko kutoka China yanaathiri biashara zetu, anasema kwasababu tulikuwa tumezoea kuuza majiko mengi hapo kabla ya wao kuja hapa. Amesema, “Hivi sasa hatuuzi mengi kama ilivyokuwa. Bidhaa zao ni rahisi sana kuliko zetu, lakini yale kutoka China si mazuri kama yetu. Ya kweli kwa kweli si mazuri.” Aliongeza.

Data za kitaifa zinaonyesha kwamba Kenya imetumia takriban dola bilioni 4 kwa kuagiza bidhaa kutoka China mwaka 2021. Kenya ni vyanzo vya wateja mbali mbali na bidhaa za aina nyingi kutoka China, wakati pia ikiuza bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 1.5 kwenye masoko ya Asia. Wafanyabiashara kama Magdalen Vivi, ambaye anauza bidhaa za jikoni zilizoagizwa kutoka nje, anasema wateja wanataka bidhaa za kisasa kama masufuria ambayo ni maarufu kama ‘nonstick’ chakula hakigandi.

“Kama ukipendekeza kuwa una masufuria ya bati, watasisitiza kuwa wanataka sufuria ‘nonstick’,” Vivi anasema “sielewi kwanini wanapendelea kuwa na sufuria kama hizo kuliko zile ambazo zinatengenezwa nchini Kenya, kwasababu kwangu mimi, sijaona sufuria zozote ambazo ni ‘nonstick’ zinatengenezwa nchini Kenya.”

Utafiti uliofanywa na Umoja wa Afrika kwa biashara ya kimataifa umegundua kuwa bara la Afrika ni soko kubwa sana kwa bidhaa za China. Baadhi ya wateja wa Kenya wanapendelea bidhaa mbali mbali ambazo ni za ubora wa kawaida. Mary Wambui ni mmoja wa wanunuzi hao.

“Siku zote kuna kuchagua kati ya bidhaa,” Wambui amesema. “Wakati wote, unapata bidhaa mpya, na wana aina tofauti. Hupati bidhaa hizo hizo kila mara. Kila wakati unapofika hapa, kuna kitu kipya kimejitokeza.”

Wohoro Ndhoho, mchumi nchini Kenya, anasema ukosefu wa teknolojia ya kisasa katika sketa ya uzalishaji nchini Kenya kuna maana kuwa bidhaa nyingi zinatengenezwa ndani ya nchi na mafundi wa nchini humo, na siyo mashine.

“Sekta ya Jua Kali nchini Kenya imekuwa ikisukumwa zaidi na nguvu ya watu na siyo mashine,” Ndhoho alisema. “Kwa hiyo, unagundua kwamba ina maana kwamba wakati vitu vinapotengenzwa nchini China, vinaweza kuwa ni kwa idadi kubwa. Ambapo kama leo ukienda Gikomba, bado utaona makarai ya kupikia mandazi yanayotegenezwa kwa mikono yao. Kwa hiyo, katika kila saa moja wanatengeneza karai moja, wakati mashine inatengeneza makarai 1,000.”

Shirikisho la Kitaifa Kenya kwa chama cha Jua Kali limeiambia VOA kwamba uagizaji bidhaa kutoka China umekuwa ni gharama kubwa kwa soko la kieneo. Mhandisi Charles Kalomba ni katibu mkuu wa chama cha mafundi.

“Majiko yanayotumia nishati chache, ambayo yamewekewa saruji ndani, yametengenezwa maalum yakiwa yamefunikwa na sarufi,” Kalomba alisema. “Tumezoea kutengeneza mengi kwa ajili ya soko la Afrika Mashariki. Leo, kuna mmiminiko mkubwa wa bidhaa kama hizo katika soko.”

Data kutoka shirika la Kenya la Export Promotion and Branding linaonyesha kwamba Afrika Kusini ni nchi pekee ya kiafrika miongoni mwa za juu 25 ambazo zinaagiza bidhaa kutoka China. Maafisa nchini Kenya wanategemea mikataba ya kibiashara kuuza zaidi kwa China. Afisa mtendaji mkuu wa shirika hilo, Wilfred Marube, anaelezea.

“Kulikuwa na mikataba ya pamoja mwezi Januari ambapo baadhi ya maeneo yalikubaliwa,” Marube alisema. “Na pia, kamati ya pamoja iliundwa kimsingi kuuliza maswali, ‘Serikali ya kichina inafanya vipi kufanya kazi pamoja kuongeza fursa ya soko kwa bidhaa za Kenya, hasa bidhaa za kilimo?”

Tiku Shah ananufaika kutokana na soko kubwa la China. Shah anauza bidhaa mpaka makontena 100 ya maparachichi kwa zaidi ya watu bilioni 1.4.

“Hivi, sasa tuna maparachihi, lakini lazimi yawe ya ubora wa hali ya juu, yawe mengi,” Shah amesema. “Wengi wetu tuko tayari kwa kiwango hicho cha biashara. Ni biashara kubwa kwa kiwango kikubwa. Kinahitaji uwekezaji mkubwa sana, na linahitaji soko lenye mwelekeo mahsusi.”

China ni ya 11 kati ya nchi zinazoongoza kwa mauzo ya nje kwa Kenya na ilichangia takriban asilimia 2.3 ya jumla ya mauzo ya nje, kwa mujibu wa takwimu za kitaifa.

XS
SM
MD
LG