Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 21:03

Marekani kuzuia ongezeko la ushawishi wa China, Rashia barani Afrika


Ushirikiano wa kijeshi kati ya Marekani na nchi za Afrika
Ushirikiano wa kijeshi kati ya Marekani na nchi za Afrika

Utawala wa Rais Donald Trump umetangaza mkakati mpya wa Marekani katika bara la Afrika ikiwa ni juhudi za kuzuia kuongezeka kwa ushawishi wa China na Rashia barani humo.

Akitangaza mkakati huo Ijumaa, mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani, John Bolton, alishambulia sera za China na Rashia kama ni za ukandamizaji na zinaiweka Afrika katika madeni.

Sera ya Marekani

Amefafanua kuwa ni kinyume kabisa na sera ya Marekani ambayo inataka kusaidia kuleta maendeleo Afrika kwa njia ya ushirikiano.

Akitangaza mkakati huo siku ya Alhamisi katika taasisi ya kihafidhina ya Heritage Foundation hapa Washington, Bolton, amesema baada ya misaada ya mabilioni ya dola ya walipa kodi wa Marekani kutolewa kwa nchi za Kiafrika hakuna mafanikio yaliyo patikana katika kuzuia ugaidi, itikadi kali na ghasia.

Bolton : Fedha hizo hazijaweza kuzuia mataifa kama China na Rashia kufaidika na utajiri wa mataifa ya Afrika kwa nguvu na maslahi yao binafsi. Na hazijapelekea kuwepo na utawala bora wenye utulivu na uwazi, ukuwaji wa kiuchumi na kuongezeka kwa maendeleo barani kote.

Masharti ya Msaada wa Marekani

Mshauri huyo wa rais anasema kuanzia hivi sasa marekani haitavumilia tena mtindo huo wa msaada usoleta tija, msaada bila ya uwajibikaji na huduma bila ya mageuzi.

Tunataka mataifa ya Afrika yafanikiwe na kuendelea kuwa huru kikweli kweli, ameeleza.

Ushirikiano mpya

Katika miezi na miaka ijayo tunania ya kufikia makubaliano ya biashara ya kisasa na yaliyo kamilika kwenye bara hilo yatakayo hakikisha mabadilishano ya haki na usawa kati ya Marekani na mataifa ya Africa, amesema Bolton.

Kabla ya kutangaza mkakati huo Alhamisi maafisa wa serikali na wachambuzi walikuwa wakiwaeleza wabunge juu ya mkakati huo mpya.

Yun Sun wa kituo cha utafiti cha Stimson Center anasema China inajiimarisha barani humo.

Stimson Center

Mchambuzi huyo wa Stimson Center amesema kuwa China inaimarisha hadhi yake kama mchangiaji wa Amani na utulivu barani Afrika, ikijionyesha kama mshikadau wakuaminika huku ikihalalisha na kupanua ushawishi wake wa kijeshi barani humo.

Anasema bajeti ya msaada wa kigeni ya Marekani kwa bara la Afrika imepunguzwa sana chini ya utawala wa Trump ikiwa ni jambo ambalo Wademokrats wanasema inapeleka ujumbe hasi.

Mwenyekiti Ed Royce

Mwenyekiti wa kamati ya masuala ya kigeni wa bunge la Marekani Ed Royce anasema kuna haja ya kuongeza bajeti hiyo ili kuweza kushirikiana vyema na Afrika.

Kwa upande wa jukumu la Marekani katika kulinda amani Afrika mshauri wa rais Bolton amesema serikali inatafakari juu ya kuondowa wanajeshi wake kutoka kikosi hicho, akisema Washington haiwezi kuendelea kuwa sehemu ya kazi isiyo na uwajibikaji.

Wazo hilo lilipendekezwa hivi karibuni na Waziri wa Ulinzi Jim Mattis kutaka kuwaondoa wanajeshi wa Marekani kutoka kikosi hicho.

XS
SM
MD
LG