Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 14:41

Marekani yawawekea vikwazo maafisa wengine wa usalama wa Iran


Raia wa Iran Ibrahim Raisi.
Raia wa Iran Ibrahim Raisi.

Marekani Jumatano iliwalenga maafisa watatu wa usalama wa Iran, na kuwawekea vikwazo vinavyohusiana na ukiukaji wa haki za binadamu, wizara ya fedha ya Marekani ilisema, ikitolea mfano ukandamizaji unaoendelea wa Tehran dhidi ya waandamanaji katika maeneo yenye Wakurdi wengi.

Vikwazo vya hivi punde zaidi vya Marekani tangu kuzuka kwa maandamano nchini kote, kujibu kifo cha mwanamke wa Kikurdi Mahsa Amini mwenye umri wa miaka 22 chini ya ulinzi wa polisi mwezi Septemba, vililenga maafisa wakuu wanaodaiwa kuhusika tika ukandamizaji uliotekelezwa na maafisa wa Iran dhidi ya maandamano katika miji ya Wakurdi, kaskazini magharibi mwa Iran, wizara hiyo ilisema.

Vikwazo hivyo viliwakumba maafisa wawili katika mji wa Wakurdi wa Sanandaj, Gavana Hassan Asgari na Alireza Moradi, kamanda wa vikosi vya sheria vya jiji hilo.

Wizara hiyo ilisema Asgari na maafisa wengine walitoa sababu ya uwongo ya kifo kwa mwandamanaji mwenye umri wa miaka 16 aliyeripotiwa kuuawa na vikosi vya usalama.

Mtuhumiawa mwingine aliyelengwa ni Mohammad Taghi Osanloo, kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu wanaosimamia mji mwingine wa Wakurdi, Mahabad, ambapo vikosi vya ziada vimetumwa kukabiliana na maandamano. Ujumbe wa Iran katika Umoja wa Mataifa mjini New York haukujibu mara moja ombi la kulizungumzia suala hilo.

XS
SM
MD
LG