Mahakama ya Iran imesema watu watano waliokamatwa katika harakati ya serikali ya kukabiliana na maandamano ya miezi miwili wamehukumiwa kifo tangu Jumapili.
Wafungwa hao watano, ambao hakuna hata mmoja wao aliyetajwa, ni pamoja na watu watatu ambao walihukumiwa kifungo hicho Jumatano.
Katika ujumbe uliotumwa kwa VOA, Mahmood Amiry-Moghaddam, mkurugenzi wa shirika la Haki za Binadamu la Oslo la Iran, alisema serikali ya Iran inatumia hukumu ya kifo kujaribu kuwatia hofu wananchi kwa mara nyingine tena kuogopa mamlaka yake.