Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 09, 2022 Local time: 16:27

Iran yawakamata raia 40 wa kigeni kwa madai ya kuhusika katika maandamano


Maandamano ya Iran, Oktoba 27, 2022. Picha ya AP

Iran, ambayo imekuwa ikiyalaumu mataifa hasimu ya kigeni kuchochea maaandamano yaliyosababishwa na kifo cha mwanamke wa Kikurdi aliyekuwa chini ya ulinzi wa polisi, Jumanne imesema raia 40 wa kigeni walikamatwa kwa kuhusika kwao katika mzozo huo.

Taifa hilo la Kiislamu limekumbwa na maandamano ya nchi nzima tangu kifo cha mwanamke wa Kikurdi Mahsa Amini mwenye umri wa miaka 22 kilichotokea Septemba 16 akiwa chini ya ulinzi wa polisi wa maadili, baada ya kukamatwa akivaa nguo “zisozofaa”, kulingana na polisi wa maadili.

Msemaji wa mahakama ya Iran Masoud Setayeshi ameuambia mkutano wa waandishi wa habari kwa njia ya televisheni kwamba “ Kufikia sasa, raia 40 wa kigeni walikamatwa kwa kuhusika kwao katika maandamano,” bila pamoja na hivo kufichua uraia wao.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG