Shirika hilo lilikuwa likizungumzia kasi ya hivi punde zaidi ya mpango wa atomiki wa Iran, licha ya pingamizi za mataifa ya Magharibi.
Kituo hicho kilichofunguliwa miaka mitatu iliyopita baada ya kuvunjika kwa mkataba wa nyuklia kati yake na madola yenye nguvu, kama vile Marekani.
Taarifa hizo ziliripotiwa kwanza na shirika la habari la Iran, ISNA na baadaye kuthibitishwa na mkuu wa shirika la nishati ya atomiki nchini humo, Mohammad Eslami.
Hatua hiyo inaonekana kuwa jibu la Iran kwa uamuzi wa wiki iliyopita wa shirika la kimataifa la nguvu za Atomiki IAEA, wa kuridhia azimio la mataifa ya magharibi lililoikosoa Tehran, kwamba haitoi ushirikiano katika kushughulikia suala la mradi wake ulioibua utata wa nyuklia. Ripoti za urutubishaji madini ya Uranium kwa asilimia 60 zinaweza kuibua wasiwasi wa kimataifa kuwa Iran inadhamiria kuunda bomu la nyuklia linalohitaji asilimia 90 pekee ya madini yaliyorutubishwa, kwa mujibu wa wachambuzio na wataalam.