Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 09, 2022 Local time: 01:08

Malawi : Majaji waanza kusoma hukumu ya kesi dhidi ya Mutharika


Majeshi ya Malawi yakiwa yanasimamia ulinzi wakati waandamanaji wakipinga madai ya jaribio la kutaka kuwahonga katika kesi inayotaka uchaguzi wa Rais wa Mei, 2019 ubalitishwe.

Majaji wa Mahakama ya Katiba ya Malawi Jumatatu wameanza kusoma uamuzi wa kesi inayosubiriwa kwa hamu ya uchaguzi uliokuwa na utata na wanaangalia iwapo ifute matokeo ya ushindi wa Rais Peter Mutharika mwezi Mei mwaka 2019.

Wachambuzi wanasema vyovyote vile mahakama itakavyochagua kuna uwezekano wa kuzuka ghasia katika taifa hilo la kusini mwa Afrika.

Kesi hiyo imelivutia taifa na kuwafanya wananchi wa Malawi kusikiliza bila ya kukosa matangazo ya stesheni za radio kwa masaa mengi wakati mashahidi wakitoa vidhibiti juu ya uchakachuaji wa kura.

Usalama umeimarishwa kwenye mahakama hiyo wakati majaji wakipelekwa kwa magari yenye uwezo wa kukinga risasi.

Helikopta ya kijeshi ilikuwa mara kwa mara inazunguka katika eneo la mahakama na eneo la wilaya la kibiashara wakati hukumu hiyo inaendelea kusomwa.

Malawi imeshuhudia maandamano ya mara kwa mara tangu Mutharika alipotangazwa mshindi mei 21 baada ya kupata asilimia 38.5 ya kura.

Mpinzani wake wa karibu Lazarus Chakwera aliyekuwa nyuma yake kwa kura 159,000 alidai kura zake kuwa zimeibiwa.

Kufuatia madai hayo chama chake cha Malawi Congress, MPC, pamoja na muungano wa upinzani wa United Transformation Movement, UTM, waliwasilisha malalamiko mahakamani kupinga matokeo hayo.

Hii ni mara ya kwanza kwa uchaguzi kupingwa mahakamani tangu taifa hilo lilipojipatia uhuru wake kutoka Uingereza mwaka wa 1964.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Abdushakur Aboud, Washington, DC.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG