Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 09, 2024 Local time: 12:43

Makampuni ya Australia kuchimba madini Tanzania


Mchimbaji wa madini kutoka Tanzania, Regina Daud (kulia) na wanawake wengine wawili wakichimba madini huko Geita, Tanzania Mei 27, 2022. Picha na LUIS TATO / AFP.
Mchimbaji wa madini kutoka Tanzania, Regina Daud (kulia) na wanawake wengine wawili wakichimba madini huko Geita, Tanzania Mei 27, 2022. Picha na LUIS TATO / AFP.

Tanzania Jumatatu imesaini mikataba yenye thamani ya dola milioni 667 na kampuni tatu za Australia, kuchimba madini nadra na yale ya grafiti, ikiwa ni sehemu ya msukumo wa rais kuharakisha mashauriano ya miradi ya madini na nishati iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu.

Katika makubaliano hayo na kampuni za Evolution Energy Minerals, Ecograf Ltd na Peak Rare Earths, Tanzania itakuwa na hisa ya asilimia 16 kutoka katika kila kampuni hizo ambazo kwa pamoja zitaendesha miradi hiyo, alisema mwenyekiti wa timu ya serikali katika mazungumzo, Palamagamba Kabudi.

Serikali ya Marekani na washirika ikiwemo Australia, ambayo mbali na China, ni mzalishaji mkubwa wa baadhi ya madini adimu, wakifanya jitihada za kupunguza utegemezi wao kwa China.

Madini adimu ya kundi la madini 17 yanayotumika katika utegenezaji wa bidhaa za elektoriniki, magari ya umeme, simu maarufu kama ‘smart phones’, nishati mbadala na vifaa vya kijeshi.

Chini ya makubaliano hayo Tanzania na kampuni ya Peak Rare Earths, itafanya uchimbaji madini eneo la Ngualla, lililoko kusini magharibi mwa Tanzania.

Kabudi alisema, kampuni ya Evolution Energy Minerals na Ecograf zitachimba madini hayo ya grafiti kutoka maeneo ya kusini na mashariki mwa Tanzania. Pia Ecograf itachimba katika eneo la kaskazini.

Madini ya Grafiti yanayotumika kwenye betri za lithiamu-ioni, yanayojulikana kama anode. Takribani asilimia 70 ya madini yote ya grafiti yanatoka China, na kuna aina nyingine chache yenye uwezo wa kufanya kazi kwenye betri kikamilifu.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG